Baada ya muda mrefu wa maswali juu ya sababu iliyomfanya msanii Baraka The Prince kutoka kwenye lebo kubwa ya muziki ambayo ilimsaini ya Rockstar4000, hatimaye mmoja wa mabosi wa lebo hiyo msanii Alikiba aweka wazi kila kitu.
Akizungumza kwenye Planet bongo ya East Africa Radio alipokwenda kutambulisha wimbo wake mpya wa 'seduce me', Alikiba amesema utovu wa nidhamu ndiyo uliomfanya Baraka ashindwe kuendelea kuwepo chini la lebo hiyo.
"Baraka hayupo Rockstar, alitoka sababu za kukiuka vitu ambavyo hakutakiwa kufanya, Baraka nimemjua baada ya kuwa naye Rockstar400, lakini kiukweli sikufurahishwa na vitu ambavyo alikuwa akifanya, nadhani nilikuwa nikiona kama ni utoto lakini si utoto tena, ni kutokuwa na heshima nikaona haina haja, na mimi nikiwa kama mtu mzima sitakiwi kugombana na mtu mdogo inatakiwa umuache dunia imfunze kidogo, au kama kuna kitu ambacho amefanya au kalishwa sumu basi akapewe dawa itoke", alisema Alikiba
Alikiba aliendelea kusema kuwa msanii huyo alichukuliwa na Rockstar4000 kwa sababu waliona ana kipaji kikubwa, hivyo wakaona ni vyema kuwa ndani ya lebo hiyo.