SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Agosti 2017

T media news

Hawa Hapa Wasanii 6 Anaowakubali Mbunge wa Nzega Bashe

Mbunge wa Jimbo la Nzega kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) Hussein Mohammed Bashe amefunguka na kutaja wasanii wake sita ambao anawakubali zaidi na kudai siku zote yeye ni mpenzi wa muziki wa hip hop.

Bashe amesema katika orodha ya wasanii ambao anawakubali na kupenda kazi zao ni pamoja na Roma Mkatoliki, Chid Benz, Prof Jay, Nay wa Mitego pamoja na Sugu alimaarufu kama Jongwe.
"Japo mimi ni mgonjwa wa muziki wa Hip hop ndiyo maana kwenye orodha yangu ya wasanii naowapenda yupo Roma, Chid Benz, Jay, Ney, Sugu ila Alikiba ni kielelezo cha msanii anayejua nini kinatakiwa mtu kuwa msanii, anaweza kuwa hana mafanikio kama wengine lakini huyu jamaa akiendelea hivi ana 'bright future' soko halitamchoka haongezi mashabiki kwa skendo, anakuza 'fan base' kwa muziki" alisema Bashe

Mbali na hilo Hussein Bashe aliendelea kumpa sifa Roma Mkatoliki na kusema tungo zake na muziki ambao unafanya unatosha kukupa picha uwezo wake na ni mtu wa aina gani kupitia tungo zake tu na kudai watu hawa wanastahili kulindwa.
"Nyimbo za Roma Mkatoliki zinataswira ya aina ya mtu na ubongo wake, sikiliza wimbo kama Mathematics, 2030 hawa ni watu wakulindwa na kuenziwa" alisema Hussein Bashe