SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Agosti 2017

T media news

TFF Kutengeneza Ngao Mpya ya Simba

Baada ya shirikisho la soka Tanzania TFF kuomba radhi kwa kutoa Ngao ya Hisani kwa Simba iliyokuwa na makosa ya kiuandishi, leo shirikisho hilo limeonesha na kutangaza kuitengenezea Ngao mpya Simba ambayo watawakabidhi siku ya mchezo wa Ligi Kuu kati ya Simba dhidi ya Azam FC.

Kama utakuwa unakumbuka TFF ambao ndio waandaaji wa mchezo wa Ngao ya Hisani kati ya Simba dhidi ya Yanga uliyochezwa uwanja wa Taifa August 23 na Simba kupata ushindi wa penati 5-4, ilitolewa Ngao ya Hisani ambayo iandikwa kimakosa ‘SHEILD’ badala ya ‘SHIELD’ lakini imesema imewaadhibu wahusika waliyofanya kosa hilo.

Hivyo TFF wamewatengenezea Ngao mpya Simba ambayo haina makosa, pamoja na hayo TFF imethibitisha nahodha wa Taifa Stars Mbwana Samatta na Elias Maguli wamewasili kambini wakati Abdi Banda ataingia mchana wa leo na Simon Msuva usiku wa leo.