SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 29 Agosti 2017

T media news

Msuva Anatarajiwa Kuwasili Usiku wa Leo

Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania na Difaa EL Jadida,  Simon Msuva anatarajiwa kuwasili nchini usiku wa leo (Jumanne) kujiunga na kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kwa mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Botswana.

Msuva ni miongoni mwa wachezaji saba wanaocheza nje walioitwa na Kocha Salum Mayanga kwa ajili ya mchezo huo wa Septemba 2 utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru.

Leo mchana kwa saa za Morocco, Msuva ataiongoza Al Jadida kuivaa FUS Rabat katika mchezo wa Ligi Kuu ya nchini 'Botola Pro League.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas alisema mchezaji huyo ataungana na wenzake ambao wameshaanza maandalizi ya mchezo huo.

"Wachezaji wa ndani wapo na Mbwana Samatta pia amewasili, leo usiku tunamtarajia Msuva kutoka Morocco," alisema Lucas.

Wachezaji wengine wanaocheza soka nje waliotwaa ni pamoja na Orgenes Mollel anayecheza FC Famalicao, Ureno na kiungo wa Sony Sugar ya Kenya, Hamis Abdallah.