SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 31 Agosti 2017

T media news

Dar yaibuka kinara kwa fursa za kibiashara Afrika

Bara la Afrika limekuwa moja ya kitovu kikubwa cha uwekezaji duniani. Baadhi ya nchi barani Afrika zimekuwa na nafasi nyingi za uwekezaji zaidi ya nyingine.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na ‘PricewaterhouseCoopers’ (PwC) imelijata Jiji la Dar es Salaam kuwa ndilo linaloongoza zaidi na kuyashinda Majiji mengine yalioendelea barani Afrika kwa kuwa na fursa nyingi za kibiashara na uwekezaji.

Ripoti hiyo imeeleza pia kuwa Jiji la Lusaka nchini Zambia linashika nafasi ya pili huku Jiji la Nairobi- Kenya na Jiji la Lagos- Nigeria yakifungana katika nafasi ya tatu.

Jiji la Accra- Ghana limeshika nafasi ya tano, Abidjan– Ivory Coast nafasi ya sita wakati Kigali ya Rwanda imeshika nafasi ya saba.

Nafasi ya nane imeshikiliwa na Addis Ababa- Ethiopia, ikifuatiwa na Kapala- Uganda na nafasi ya kumi inashikiliwa na Jiji la Cairo- Misri.

Sababu tano zilizotajwa kuwa chanzo cha Majiji haya kuwa na fursa mbalimbali za kibiashara zaidi ya mengine ni pamoja na uwepo wa soko kubwa la walaji, teknolojia, huduma nzuri za kifedha, utalii pamoja na ubora wa miundo mbinu.

Mambo mengine yaliyoangaliwa katika ripoti hii kuwa ni kichocheo cha uwepo wa nafasi nyingi za kibiashara ni pamoja na ripoti ya miundombinu, nguvu kazi, uchumi, pamoja na idadi ya watu.