Serikali wilayani Kilombero imepiga marufuku usafirishaji mpunga kwenda maeneo mengine,badala yake waukoboe na kusafirisha mchele ili kuongeza thamani ya zao hilo.
Marufuku hiyo imeelezwa inalenga kuwawezesha wakulima kunufaika na kilimo cha mpunga, kujikwamua na umasikini na kukuza uchumi.
Mkuu wa Wilaya ya Kilombero, James Ihunjo amesema hayo baada ya kuzungumza na wadau wa kilimo cha mpunga wakiwemo wakulima kutoka wilaya za Mvomero,Kilombero,Ulanga na Malinyi pamoja na mashirika na taasisi zinazojihusishana kusaidia wakulima wa zao hilo.
Ihunjo amesema wilayani mwake wameweka vizuizi viwili kudhibiti wafanyabiashara wanaokaidi agizo hilo.
“Mpunga unaouzwa lazima uchakatwe ili kuongeza thamani jambo linalomfanya mkulima aweze kufaidika,”amesema