SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 28 Agosti 2017

T media news

Tundu Lisu Apingwa Mgomo wa Mawakili Nchi Nzima

Wakili wa kujitegemea na mmiliki mwenza wa Smile Stars Attorneys, Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito uliotolewa na Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kutaka wanachama wote wa TLS kususia kwenda mahakamani kwa siku mbili.

Akiongea na waandishi wa habari Leonard Tungaraza Manyama amepinga wito huo na kuwataka Wanachama wote wa TLS kuendelea na shughuli zao kama kawaida na amewataka watendaji wa TLS kutoigeuza taasisi hiyo kama chama cha siasa au taasisi inayoendesha shughuli zake kwa mtindo wa kiharakati na badala yake kibaki kwenye majukumu yake ya kutoa huduma kama taasisi ya kitaaluma.

Aidha Manyama amesema yeye kama mwanasheria na mwanachama wa TLS, amesikitishwa na tukio la shambulizi kwenye ofisi za IMMMA Advocates na kuitaka TLS kutoa muda kwa vyombo vya dola kuendelea na uchunguzi wa tukio hilo.

Mbali na hilo Manyama amedai mawakili na wanasheria ni watumishi wa idara ya mahakama na kwamba tukio lolote la kutofanya kazi katika siku mbili hizo kutaleta usumbufu mkubwa kwa wananchi wa kipato cha chini ambao wamekuwa wakihangaika kutafuta haki zao kwa muda mrefu, huku mpango wa kuhakikisha kesi za muda mrefu zinapunguzwa mahakamani nao ukikwama.

Leonard Tungaraza Manyama ameibuka siku moja baada ya Rais wa TLS  Tundu Lissu kuwataka mawakili kutohudhuria kwa siku mbili shughuli za mahakama Jumatatu na Jumanne kama ishara ya kulaani tukio la shambulizi lililofanywa kwenye ofisi za kampuni ya mawakili ya IMMMA