SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 30 Agosti 2017

T media news

Bado Naipa Nafasi Yanga ya Kutetea Ubingwa - Msuva

LICHA ya Yanga kuanza ligi kwa sare, lakini kiungo wa zamani wa timu hiyo, Simon Msuva, ameibuka na kusema kuwa, bado anaipa timu hiyo nafasi ya kutetea ubingwa wake msimu huu.
Yanga ambayo ni bingwa mtetezi wa ligi hiyo, Jumapili iliyopita ilitoka sare ya bao 1-1 na Lipuli FC, huku wapinzani wao wa jadi, Simba wakianza kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

Msuva ambaye kwa sasa amejiunga na Klabu ya Difaa Al Jadida ya Morocco, amesema kuanza taratibu kwa Yanga hakumaanishi moja kwa moja kwamba haiwezi kutetea ubingwa wake, bali nafasi ya kufanya hivyo ipo tena kubwa.

“Nimefuatilia mechi za mwanzo za ligi ya Tanzania na nimesikia Simba wameanza kwa kushinda 7-0, wakati timu yangu ya zamani ya Yanga ikitoka sare, watu wengi wanasema Simba itakuwa bingwa, lakini binafsi naona Yanga ndiyo yenye nafasi ya kufanya hivyo tena.

“Nasema hivyo kwa sababu ukiangalia kweli zote zimefanya usajili wa maana, lakini Yanga ina wachezaji wengi waliokaa pamoja na kuzoeana tofauti na Simba yenye sura nyingi mpya. “Lakini pia, Donald Ngoma amerejea vizuri, na yule kiungo mkabaji waliyempata (Papy Tshishimbi), nadhani lile tatizo la siku nyingi limepata mtu sahihi wa kulitibu,” alisema Msuva.