Siwezi Jifananisha na Lulu Diva : Malaika

Msanii wa Bongo Flava, Malaika amesema hawezi kujilinganisha na Lulu Diva kwani kila mmoja anafanya aina yake ya muziki.

Hata hivyo ameeleza kuwa Lulu Diva ni msanii mpya ambaye pia anafanya vizuri, hivyo wale wanaowalinganisha hawafanyi kitu kibaya.

“Sijui, siwezi kujilinganisha, ni watu ambao wanaona ndio wanaweza kutulinganisha lakini naweza kusema Malaika ni Malaika. Ukinisikiliza vizuri katika miziki yangu and the way navyotunga,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“Sijafanikiwa sana kusikiliza miziki yake lakini najua ule mmoja ‘Usimuache’, kwa hiyo najua yupo tofauti na mimi, aidha kuna vitu anapenda kutoka kwangu. Unajua kuna mtu anaweza kuwa ni fan mpaka anafanya vitu kama wewe, so inawezekana pia yupo hivyo,” amesisitiza.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA