Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2017

Breaking News: Mtokeo ya Kidato cha Nne 2016 Yametoka......Bofya Hapa Kuyatazama

Picha
Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limetangaza matokeo ya kidato cha nne mwaka 2016 ambapo umefaulu wa jumla umeongezeka kwa 2.56% kutoka 67.53% mwaka 2015 hadi 70.09% mwaka 2016. Katibu Mtendaji wa barza hilo, Dkt Charles Msonde amesema kati ya wanafunzi 408,372 waliofanya mtihani, jumla ya wanafunzi 277,283 wamefaulu, wakiwemo wasichana 135,859 sawa na asilimia 67.06 na wavulana 141,424 sawa na asilimia 73.26. Kwa upande wa watahiniwa wa shule, Dkt Msonde amesema kuwa 244,762 sawa na asilimia 70.35 ya waliofanya matihani wamefaulu ikilinganishwa na wanafunzi 240,996 sawa na asilimia 67.91 waliofaulu mwaka 2015. Kwa upande wa ubora wa ufaulu, amesema watahiniwa wa shule wenye ufaulu mzuri wa Daraja la kwanza hadi la tatu ni 96,018 sawa na asilimia 27.60 ==>>Bofya  <<HAPA>  Kuyaona Matokeo ya Kidato cha Nne ==>Bofya <<HAPA> Kuyaona  matokeo ya mtihani wa maarifa (QT) 2016 

Mhubiri Aliyekuwa na Wake 86 Afariki Nigeria

Picha
Mhubiri mmoja wa zamani wa Kiislamu nchini Nigeria ambaye alikuwa na takriban wanawake 86 ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 93. Mohammed Bello Abubakar alifariki nyumbani kwake katika jimbo la Niger siku ya Jumamosi, kutokana na ugonjwa ambao haukutajwa Watu wengi walihudhuria mazishi yake siku ya Jumapili. Gazeti la Nigeria la Daily Trust liliripoti kuwa alipokuwa na wake 86 mwaka 2008 wakati aliangaziwa na vyombo vya habari, idadi hiyo ilipanda hadi wake 130 wakati wa kifo chake. Wengine wao walikuwa wajawazito. BBC iliripoti mwaka 2008 kuwa alikuwa na takriban watoto 170 lakini gazeti hilo lilisema kuwa aliwaacha watoto 203.

Raia Marekani Waendelea na Maandamano Kumpinga Trump

Picha
Wengi wanasema dini isiwe sababu ya kubaguliwa Raia nchini Marekani bado wanaendelea na maandamano ya kupinga amri ya kiutawala iliyotolewa na Rais Trump inayozuia kwa muda raia wanaotoka mataifa saba ya kiislamu kuingia nchini Marekani. Hata hivyo, tangu hatua hiyo kutolewa, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa raia wa nchi mbalimbali huku baadhi wakiunga mkono hatua hiyo, na wengine wakiipinga vikali kwa kusema kuwa ni makosa watu kubaguliwa kutokana na imani zao za kidini. Wakati huo huo, Kaimu mwanasheria mkuu nchini Marekani ameamuru idara ya wanasheria kutoitetea mahakamani amri hiyo. Sally Yates, ambae aliteuliwa na Barack Obama, amesema bado hajashawishika kwamba inaruhusiwa kisheria. Waandamanaji wanasema hatua hiyo ni kukiuka haki za binaadam Baadhi ya wanadiplomasia wa Marekani wameandika waraka unaopinga amri hiyo, ambapo wamesema katu haitaifanya Marekani kuwa salama. Lakini msemaji wa Rais amewajibu kwa kuwaambia, wafuate amri hiyo au waondoke. Nae aliyeku...

VIKAO VYA BUNGE KUANZA LEO

Picha
Mkuu wa Kitengo cha Habari, Elimu na Masiliano Ofisi ya Bunge, Owen Mwandumbya akizungumza na wanahabi mjini Dodoma jana akitoa taarifa ya yale yatakayojiri katika Mkutano wa sita wa Bunge la 11 unaotaraji kuanza leo Januari 31 hadi Februari 10 mwaka huu mjini Dodoma. Mkutano wa Sita wa Bunge unatarajiwa kuanza siku ya Jumanne tarehe 31 Januari 2017 na kumalizika tarehe 10 Februari 2017 Mjini Dodoma.  Mkutano huo utakuwa ni mahususi kwa ajili ya kupokea Taarifa za mwaka za Kamati za Kudumu za Bunge ambapo Kamati 14 za kisekta na mtambuka zitawasilisha taarifa zake Bungeni katika kipindi hiki. Shughuli nyingine zitakazofanyika katika Mkutano huu ni kama ifuatavyo:- 1.0 KIAPO CHA UAMINIFU Kufuatia uteuzi wa wabunge watatu walioteuliwa na Mhe. Rais Dk. John Pombe Magufuli hivi karibuni na Uchaguzi Mdogo uliofanyika katika Jimbo la Dimani, Zanzibar Tarehe 22 Januari 2017, kutakuwa na Kiapo cha Uaminifu kwa Wabunge wapya wanne ambao ni:- (i) Mhe. Alhaji Abdallah Majula Bulembo (i...

Serikali Kutoa Majibu Juu ya Hali ya Chakula Nchini Leo Bungeni..!!!

Picha
MKUTANO wa Sita wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaanza leo mjini Dodoma. Serikali inatarajiwa kutoa kauli mbili kuhusu hali cha chakula nchini na deni la Taifa linaloenda sanjali na hali uchumi nchini. Akizungumza na vyombo vya habari mjini Dodoma jana, Mkurugenzi wa Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, Owen Mwandumbya alisema pamoja na kauli hizo za serikali, kabla yake kutakuwa na kauli ya Spika wa Bunge, Job Ndugai ambazo zitatolewa kabla ya kipindi cha maswali na majibu. Katika kikao cha leo, kutakuwa na kiapo cha uaminifu wabunge watatu wa Kuteuliwa na mmoja wa kuchaguliwa ambao ni Abdallah Bulembo, Profesa Palamagamba Kabudi na Anne Kilango Malecela (wote wa Kuteuliwa) na mbunge wa kuchaguliwa kutoka Jimbo la Dimani Zanzibar, Ali Juma Ali (Dimani-CCM). Katika mkutano huo, Kamati 14 za kisekta zitawasilisha taarifa mbalimbali ambazo zitajadiliwa na wabunge kadiri ratiba itakavyokuwa inaelekeza siku hiyo. Aidha, katika mkutano huo, itawasilishwa misaada ...

Hii ni zaidi ya Laana,Diamond na Ali Kiba Wakimbia Mwaliko wa Kuhudhuria Maulidi ya Kuzaliwa Mtume Muhammad(S.A.W),Shehe Mkuu Dar Atoa Kauli Hii..!!!

Picha
Ama kweli imeshangaza wengi! Kitendo cha nyota wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ na Ally Saleh Kiba  kushindwa kutokeza kwenye sherehe za kumbukumbu ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W), yaani Maulidi iliyofanyika wilayani Temeke jijini hapa ambapo walialikwa na Shehe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum na kumuahidi kuwa wangefika. Katika Maulidi hiyo ambayo ilifanyika Mtaa wa Liganga wilayani hapo na mwenyeji wa shughuli hiyo kuwa Shehe Alhad, ilihudhuriwa na waheshimiwa mbalimbali wakiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd, Makamu wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, Mufti wa Tanzania, Shehe Abubakar Zubeir na wengineo. KAULI YA SHEHE MKUU JUKWANI Wakati Maulidi hiyo ikiendelea, Shehe Alhad aliutangazia umati uliojaa kuwa, katika hafla hiyo aliwaalika wasanii mbalimbali na kuwataka watu kuwachukulia wasanii hao kama wenzao. Akiendelea kuweka mambo sawa, alisema mpaka muda huo msanii ambaye alishafika n...

Katibu Mkuu Umoja wa Matifa Amwakikishia Rais Magufuli Ushirikiano ..!!

Picha
KATIBU Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Antonio Guterres amemhakikishia Rais John Magufuli kuwa UN itaimarisha ushirikiano wake na Tanzania katika kutekeleza majukumu mbalimbali, hususan tatizo la wakimbizi. Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa, Guterres alisema hayo jana, alipokutana na Rais Magufuli kando ya Mkutano wa 28 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU), unaoendelea mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Guterres aliahidi kuwa UN itaongeza ushirikiano na Tanzania na kwamba itatia msisitizo zaidi katika kukuza wadau mbalimbali wa maendeleo ndani ya jumuiya ya kimataifa, kuchangia juhudi zinazofanywa na Tanzania katika kuwapa hifadhi wakimbizi wa nchi mbalimbali tangu mwaka 1971. Kwa upande wake, Rais Magufuli alimpongeza Guterres kwa kuchaguliwa kwake hivi karibuni kushika wadhifa huo. Alisema Tanzania itaendelea kushirikiana kwa karibu na Umoja wa Mataifa. Rais Magufuli pia alimweleza Katibu Mkuu huyo wa UN juhudi mbalimbal...

Beyonce Apigwa Mimba ya Pili.

Picha
Imethibitika kuwa mwanamuziki wa R&B, Beyonce Knowles ana mimba ya miezi minne baada ya kipande cha video kusambaa kikionesha mimba hiyo. Kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa Showbiz, umeanika kipande hicho cha Beyonce na kueleza kuwa, staa huyo anayetamba na Albamu ya Lemonade anatarajia kupata mtoto wa pili kwa mumewe, Shawn Carter ‘Jay Z’ na hakutaka kuweka hadharani hadi atakapokaribia kujifungua. Katika kipande hicho alichoachia mtandaoni na kufuta haraka, kinamuonesha Beyonce akiwa katika kampeni ya mavazi yake aliyoyaita jina la mtoto wake, Blue Ivy yanayotambulika kama Ivy Park. Mashabiki wake wengi wa kwenye mitandao ya kijamii ikiongozwa na Twitter wamempongeza Beyonce na ujauzito huo. Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za ujauzito wake japo hakukuwa na picha zilizoonesha na sasa imeonekana wazi.

Ulishajiuliza Unapenda Nini Kwa Mpenzi Wako ?

Picha
Leo kwenye safu hii nimekuja tuongelee suala hili la wapenzi kupendana na kufikia kuwa mwili mmoja je, umewahi kujiuliza maswali kuhusiana na mwenza wako? Maswali haya yanawahusu wote. Mnatafuta nini ndani ya wenza wenu ni kitu gani mnaangalia/mnakiona ndani ya mtu unayeamua kuwa naye kama mchumba/mume/mke. Je, ni macho yake au tabasamu, ama ni muonekano wake, uchangamfu au upole, ni kitu gani unachokiona ndani ya mtu kinachokuvutia. Wengine wanavutiwa jinsi mtu anavyofikiria, au mwili wake, wewe je? Unaweza ukawa umevutiwa na kitu kimojawapo, lakini unajua uhusiano mzuri haujengwi na vitu hivi tu, kuwa na uhusiano mzuri na mwenza wako inahusisha vitu vingi sana tofauti na tabasamu lake iwe unatafuta mtu wa kuwa naye au kama tayari upo katika uhusiano hakikisha mnakubaliana vitu muhimu ambavyo mkividharau kisa umempenda kwa sababu ya shepu yake au ucheshi wake vinaweza kuharibu uhusiano huko mbele ambapo ni pagumu zaidi. Vitu unavyotakiwa kuangalia zaidi Hivi ni baadhi ya vitu una...

Breaking News..Kocha wa Simba Afunguka Mazito Juu ya Hali ya Timu Yake,Awatolea Povu Mashabiki ..!!!

Picha
KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameshusha presha ya mashabiki wa timu hiyo kwa kuwataka kuwa watulivu kwa kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha makosa yao na kutimiza lengo ambalo ni ubingwa. Simba inashika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Yanga, baada ya Jumamosi kufungwa bao 1-0, na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu, ya Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam. Yanga imekamata usukani baada ya kuifunga Mwadui ya Shinyanga juzi kwa mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 na kuiondoa Simba kileleni ambayo ina pointi 45 baada ya kipigo cha Jumamosi. Akizungumza  Omog, ambaye amekuwa katika wakati mgumu kufuatia kipigo hicho alisema hata yeye pamoja na wachezaji wameumizwa na matokeo hayo, lakini mpira ni mchezo wa makosa na kilichobaki kwa sasa ni kujipanga upya ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyokusudia mwishoni mwa msimu huu. “Hakuna anayependa kufungwa au kutolewa kwenye nafasi nzuri , lakini mashabiki wanapaswa kujua Simba siyo lazima kila siku ishinde...

Huyu Ndiye Trump Bana.. Amtimua Kazi Mwanasheria Mkuu wa Serikali Baada ya Kupinga Mpango Wake wa Kuwazuia Waislamu Wasiingie Marekani..!!!

Picha
Rais wa Marekani Donald Trump amemfuta kazi kaimu mwanasheria mkuu Sally Yates saa chache tu baada ya kuwaagiza mawakili wa idara ya haki nchini humo kutotetea uamuzi wa kuwawekea vikwazo raia wanaotoka katika baadhi ya mataifa ya kiislamu. Taarifa ya Ikulu ya Whitehouse imemshtumu kwa usaliti. Sally Yates ambaye aliteuliwa na Obama alisema kuwa hafikirii kwamba marufuku hiyo ya muda kwa raia wa mataifa saba ya Kiislamu ni halali. Wadhfa wake umechukuliwa na kiongozi wa mashtaka katika mahakama ya kijimbo huko Virginia Dana Boente. Agizo hilo la rais lililotiwa saini Ijumaa iliopita limesababisha maandamano nchini Marekani na ughaibuni. Awali kundi moja la wanadiplomasia liliandika barua likikosoa agizo hilo wakisema litazidi kuhatarisha usalama wa taifa hilo.

MOSE IYOBO AJITETEA KUHUSU KAULI YAKE YA KUMWITA HARMORAPA NYANI

Picha
Moja kati ya story ambazo zimetrend kinoma noma kuanzia asubuhi ya jana mpaka leo hii ni kuhusu kauli ya dancer wa Diamond Platnumz Mose Iyobo kumwita Harmorapa Nyani Kauli ambayo ilichukuliwa kama udhalilishaji kwa rapper huyo na kuwafanya wengi kumtolea mapovu dancer huyo na wengine  kufika mbali zaidi hadi kumfananisha na Sokwe. Soudy Brown ameamua kupiga story na Mose iyobo na kujua nini kilijiri mpaka kutokea kwa  yote hayo, je ni account yake ilihakiwa? Au ni nini kilitokea? Majibu yote yapo kwenye U-heard ya leo January 30 ambayo nimeikusanya na kukuwekea hapa kwenye video hii hapa chini.

Afariki kwa Kipigo Baada ya Kufumaniwa Akila Raha na Mke wa Mtu,Stori Kamili Hii Hapa..!!!!

Picha
WATU watatu wilayani Igunga mkoani Tabora wamekufa akiwemo mwanaume aliyeuawa na kundi la wananchi baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. Watoto wawili wa familia moja wamepoteza maisha kwa kuzama kwenye shimo la maji. Akizungumza jana mjini Tabora, Kamanda wa Polisi wa Mkoa, Kamishna Msaidizi Hamisi Selemani amesema katika tukio la Januari 28, mwaka huu katika Mtaa wa Stoo, Kata ya Igunga Mjini, mkazi wa Mtaa wa Masanga, Khalid Kassim (50) aliuawa na kundi la wananchi zaidi ya 100 ikidaiwa alifumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu. Kamanda Selemani amefafanua kuwa Kassim alifumaniwa na mwenye mke, Muungano Isaack (44) mkazi wa Mtaa wa Stoo. Amesema baada ya kumfumania, Isaack alipiga kelele kuomba msaada, ndipo wananchi walitoka kwa wingi na kumshambulia kwa kipigo Kassim. Amebainisha kuwa polisi walipata taarifa na kufika katika mtaa huo na kukuta wananchi wakiwa wamekimbia, hivyo askari walimchukua mtuhumiwa na kumpeleka Hospitali ya Wilaya ya Igunga ambako aliaga...

Mwili wa Mwanafunzi Waopolewa Ziwani

Picha
Mwili wa mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Sekondari ya Chato mkoani Geita, Shilinde Nicolaus (18) umeopolewa Ziwa Victoria baada ya kuzama Januari 28 saa tisa alasiri alipokuwa akivua na wenzake. Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo alisema  mwili huo ulipatikana juzi baada ya jitihada za wavuvi wa eneo hilo kwa kushirikiana na wananchi. Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Muungano lilipotokea tukio hilo, Kapembe Charles alisema kijana huyo na wenzake ambao walinusurika, walipata ajali hiyo  baada ya mtumbwi wao kupigwa na dhoruba kisha kuzama. Charles alisema katika tukio hilo wenzake wawili, Daud Deus na Mgonyolo Hamis wote wakazi wa Kijiji cha Kitela walinusurika  baada ya kuogelea hadi nchi kavu. Mmoja wa wanafunzi hao, Daud Deus alisema wakati wakiendelea  kuvua, kulikuwa na upepo mkali uliosababisha mtumbwi wao kuzama. “Mimi na Hamis tulifanikiwa kuogelea kwenye majani yaliyoota ndani ya maji, kisha tukaokolewa na wavuvi,” ...

MREMBO GIGY MONEY ADAI MABWANA WA WEMA SEPETU WAMEANZA KUMSHOBOKEA

Picha
Kufuatia kusambaa kwa video yake akifanya vitendo vya kifuska hadharani na aliyekuwa mpenzi wa staa wa sinema za Kibongo, Wema Isaac Sepetu, Ibrahim Mgimbu ‘Calisah’ mwanadada anayeuza nyago kwenye video za Bongo Fleva, Gift Stanford ‘Gigy Money’ amefunguka na kusema wenyewe ndiyo wanaomshobokea.  Video hiyo chafu ya Gigy na Calisah ilisambaa hivi karibuni kwenye mitandao ya kijamii ambapo watu wengi walionekana kumshangaa mwanadada huyo huku wakimtolea maneno ya kejeli kuwa hajatulia na amekuwa akipenda kuwa kimapenzi na wanaume waliopitia kwa Wema akiwemo Idris Sultan. Baadhi ya mashabiki waliozungumza na Wikienda walifunguka kuwa, Gigy anatakiwa kubadilika kwani amekuwa mtu wa matukio kila siku na amekuwa akipita kule alikopita Wema kwa sababu alianza na Idris na sasa Calisah. “Hivi Gigy haoni wanaume wengine hadi ajibebishe kwa wale ambao tayari walishakuwa na uhusiano na Wema? Hata sielewi Gigy anajisikiaje maana hii video yake na wanafanya vit...

CCM - Chadema Wanasababisha Migogoro ya Ardhi..!!!

Picha
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Wilaya ya Monduli mkoani Arusha, Loota Sanare amesema halmashauri ya wilaya hiyo inayoongozwa na Chadema, inachochea migogoro ya ardhi na chama hakitakaa kimya kwa hilo. Sanare alisema hayo juzi katika mkutano wa hadhara wa kijiji cha Lendikinya, uliohudhuriwa na vijana wa jamii ya Kimasai (morani) na wazee wa mila (Laigwanani) zaidi ya 300, kueleza ardhi ya kijiji hicho inayotaka kunyang’anywa na halmashauri hiyo. Alisema vijana wa kimorani, Laigwanani na watu wengine akiwemo yeye mwenyewe Sanare, wanamiliki ardhi iliyopo katika kijiji hicho kwa kufuata michakato yote ya kisheria na hatimaye kupata hati ya kumiliki ardhi. Alisema amesikitishwa na kauli ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli, Isack Joseph kutangaza baadhi ya watu kuwa wanamiliki ardhi katika msitu huo kinyume cha sheria. Alisema CCM haitavumilia uchochezi unaofanywa na baadhi ya viongozi wa halmashauri kwa maslahi binafsi. Pia, alisema CCM haitavumilia ku...

MUONEKANO MPYA WA RAY C,MASHABIKI WAFUNGUKA LIVE

Picha
Mashabiki wamjia juu Ray c... Wamwambia aache Diet ya kupungua mwili kwani ameanza kuharibika na kukonda...!! Wamtaka aache mara moja.

Pitia Vichwa vya Magazeti ya Leo 31/1/2017..!!!

Picha

HEART TOUCHING STORY 💓MAMA💖 Binti mmoja alizaliwa na kulelewa na Mama ambaye ni kichaa

Picha
💓MAMA💖 Binti mmoja alizaliwa na kulelewa na Mama ambaye ni kichaa wale wakuzunguka na kuokota vitu barabarani, pamoja na ukichaa wake lakini yule mama alimlea vizuri binti yake akimpa chakula mpaka alipofikia umri wa kwenda shule. Kwa bahati nzuri yule binti alipata msamaria mwema ambaye alimsomesha, ingawa yule msamaria mwema alijaribu kumchukua yule Mama na kukaa naye lakini haikusaidia. Kila aliporudishwa nyumbani siku mbili alirudi mtaani kuokota makopo na kula matakataka. Pamoja na ukichaa wake lakini kila siku ilikuwa ni lazima kwenda kwenye ile nyumba alikokuwa akilelewa binti yake kumsalimia na kila siku alikuwa akibeba chakula kwaajili ya binti yake. Ili binti yule ale kile chakula illibidi kila siku kumuwekea chakula kizuri kwenye mfuko na pale alipokuwa akiomba basi walimpa kile chakula na yeye kabla ya kula alimletea binti yake. Maisha yaliendelea hivyo mpaka binti alipoenda chuo ndipo Mama alibaki mpweke akizunguka zunguka tu mtaani. Kule chuoni binti alifanya viz...

BREAKING NEWS: Mwenyekiti wa CCM Mbeya anusurika kuuawa kwa Risasi

Picha
Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini, Efrahim Mwaitenda mwenye umri wa miaka 60 amejeruhiwa kwa kupigwa risasi mgongoni na mtu au watu wasiofahamika.   Mwenyekiti wa CCM Mbeya Mjini (Aliyekaa) akipeleka hospitali) Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Emmanuel Lukula amesema tukio hilo limetokea mnamo tarehe 29.01.2017 majira ya saa 05:45 usiku katika kitongoji cha Ilopa, Kijiji cha Mahenge, Kata ya Makwale, Tarafa ya Ntebela, Wilaya ya Kyela, Mkoa wa Mbeya. Amesema tukio hilo limetokea wakati akiwa amelala kitandani nyumbani kwake Ntembela ambapo mbinu iliyotumika ilikuwa ni  kukata wavu wa dirisha na kumjeruhi kwa kutumia silaha za kienyeji zinazotumia risasi za gololi. Mwenyekiti huyo amefikishwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya na hali yake inaendelea vizuri. Lukula amewaambia waandishi wa habari kuwa nia ya shambulizi hilo ilikuwa ni kutaka kuumua na kwamba juhudi za kuwatafuta na kuwakamata wahusika zinaendelea 

WATU ZAIDI YA LAKI TISA WASAINI KUPINGA ZIARA YA TRUMP HUKO UINGEREZA

Picha
Zaidi ya watu 900,000 wamesaini petition ya kutaka kusitishwa kwa ziara ya Donald Trump nchini Uingereza kufuatia uamuzi wake wa kupiga marufuku waislamu kuingia Marekani. Na sasa wabunge wa House of Commons watalazimika kujadili ziara hiyo. Mipango ya Trump kuzulu nchini Uingereza, ilitangazwa saa 48 zilizopita baada ya waziri mkuu, Theresa May kueleza kuwa Rais huyo ameukubali mwaliko toka kwa malkia. Petition hiyo inadai kuwa Trump hapaswi kualikwa nchini humo kuepuka kumdhalilisha malkia. Uamuzi wa Trump kuzuia raia wa nchi 7 za Kiislamu kuingia nchini Marekani umepingwa vikali.

Waziri Mkuu Atua Dodoma Kwa Ndege ya Abiria

Picha
Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewasili mkoani Dodoma leo asubuhi kwa ajili kuhudhuria vikao vya bunge  ambavyo vinatarajiwa kuanza kesho Jumanne Waziri Mkuu ameongozana na mkewe Mary Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali ambao wametumia usafri wa ndege ya abiria ya ATCL inayopitia Dodoma kuelekea Kigoma Katika Uwanja wa Ndege Waziri Mkuu amepokelewa na mkuu wa mkoa wa Dodoma Jordan Rugimbana pamoja na viongozi wa serikali na chama wa mkoa wa Dodoma Vikao vya Bunge vinaanza kesho baada ya wiki mbili za shughuli za kamati za kudumu za Bunge, na sasa tayari wabunge wamekwishawasili Dodoma kwa ajili ya vikao hivyo vitakavyodumu kwa takriban wiki 2

Bilionea wa Facebook Anataka Nawe Ufanikiwe Kama Yeye..!!

Picha
NIANZE kwa kukubaliana na wasomaji ambao wamekuwa wakilalamika kuyumba kiuchumi kwani hata mimi ninapitia kipindi kama hicho. Lakini cha msingi tusikate tamaa, tuendelee kukaza kwa kufanya kazi kwa bidii. Tusisahau ubunifu na kukipenda kile tunachokifanya ambacho mwisho wa siku ndicho kinatupatia mkate wetu wa siku. Baada ya kusema hayo, bila shaka utakuwa umewahi kutumia au kusikia Mitandao ya Kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram. Mmoja wa wamiliki wa mitandao hiyo anajulikana kwa jina la Mark Zuckeberg, Mmarekani aliyezaliwa huko White Plains, New York nchini Marekani. Jamaa ni bilionea mwenye pesa ndefu ambazo zimemfanya ashike namba tano huku akiwa na utajiri wa dola bilioni 55 (zaidi ya trilioni 110), ndiye tajiri mdogo zaidi akiwa na umri wa miaka 32. Mkewe anaitwa Priscilla Chan mwenye umri wa miaka 30. Jamaa ametajirishwa na Mtandao wa Facebook. Hakuzaliwa akiwa tajiri, aliangalia dunia inahitaji nini, hivyo akachangamkia fursa. Ni mambo yaleyale ambayo nimekuwa nikiya...

Picha: Meli kubwa ya kisasa ya Azam yatia nanga Bandari ya Tanga kwa mara ya kwanza

Picha
Meli mpya na ya kisasa iitwayo AZAM SEALINK 2 aina ya RORO yenye uwezo wa kubeba abiria wapatao 1650, mizigo uzito wa tani 717 sambamba na magari 150 imetia nanga  Bandari ya Tanga leo. Meli hiyo inatarajiwa kufanya safari zake na kutoa huduma za kubeba abiria na mizigo ikiwemo magari kutoka Pemba kwenda Unguja hadi Tanga mara moja kwa wiki.