SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Ijumaa, 27 Januari 2017

T media news

BAADA YA HARMORAPA SASAAIBUKA CHIBURAPA MTAZAME HAPA


MWEZI Januari mwaka huu katika mitandao ya kijamii aliibuka msanii chipukizi wa Bongo Fleva anayefanana sana kwa sura na msanii kutoka Wasafi Classic Baby (WCB) aitwaye Harmonize kiasi mashabiki  walimbatiza jina la ‘Pacha wa Harmonize’ au Harmorapa.  Mwanzoni mwa wiki hii ameibuka msanii mwingine anayefanana na Diamond Platnumz naye kupewa jina la Chibu Rapa. 

Katika mitandao ya kijamii msanii kutoka WCB ‘Harmonize ‘ alimuanika na baadae kumtoa kijana huyo aliyefanana na Diamond huku mashabiki wakifunguka kwa kuachangia hoja na wengi walikubaliana na Harmonize kuwa ni kweli kijana huyo amefanana kwa muonekano na  na Diamond Platnumz.

Aidha bado haijafahamika kama kijana huyo naye anafanya sanaa ya muziki au laa.