Kocha wa klabu ya Manchester United, Jose Mourinho amefunguka kuwa atamzuia nahodha wa timu hiyo Wayne Rooney endapo atataka kwenda kucheza katika ligi ya China.
Akiongea na waandishi wa habari Alhamisi hii kabla ya mchezo wao wa kombe la ligi dhidi ya Hull City, Mourinho alisema hata yaunga mkono mawazo ya mchezaji huyo endapo akifikiria kujiunga na ligi hiyo ambayo kwa sasa imeonekaa kuwavutia wachezaji wengi kutokana na fedha wanayolipwa nchini humo.
“Hii ni endapo tu mchezaji huyo ataona kuwa ana sababu ya kufanya hivyo na kuamua kuondoka United ni sawa,” amesema Mourinho.