SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 28 Januari 2017

T media news

Bond Alilazimika Kwenda Rehab Kusaidiwa Kuachana na Matumizi ya Mirungi na Pombe Ili Asimkose Wastara

Msanii wa filamu Wastara Juma amefunguka kwa kudai kuwa moja kati ya vitu ambavyo vilichangia akaachana na mpenzi wake wa sasa Bond Bin Sinan na kwenda kuolewa na mwanaume mwingine, ni matumizi ya mirungi pamoja na pombe.

Hatua hiyo ilimfanya Bond kujiuliza mara mbili mbili na ndipo alipoamua kwenda rehab kuachana na ulevi huo ili apate nafasi ya kurudi kwa malkia huyo wa filamu.

Wastara alidai ulevi huo wa Bond ulimkosesha raha ya kuamua kumuacha ili aendelee na maisha yake.

“Ukweli ni kwamba kuna issue nzito ilitokea kati ya mimi na Bond mpaka Bond mwenyewe aliamua kutoa ushuhuda na kutubu juu ya matumizi ya dawa za kulevya aina ya mirungi,” Wastara alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.

“Mpaka aliamua kuondoka mwenyewe kwenda mbali na mazigira ambayo mimi nilikuwa naishi, alikuwa anatafuta njia ya kujisaidia ili aache vile vitu ambavyo binafsi nilikuwa sivipendi,” aliongeza Wastara.

Muigizaji huyo amedai baada ya tukio hilo alishauriwa na ndugu zake kuolewa na Mbunge wa jimbo la Donge, Sadifa Khamis Juma lakini ndoa hiyo haikudumu wakaachana.

Kwa sasa Bond na Wastara wamerudiana na wanaendelea na mahusino yao baada ya Bond kufanikiwa kuachana matumizi hayo ya Madawa ya kulevya aina ya mirungi.

Pia Bond kwa sasa ni meneja wa muigizaji huyo.