Imethibitika kuwa mwanamuziki wa R&B, Beyonce Knowles ana mimba ya miezi minne baada ya kipande cha video kusambaa kikionesha mimba hiyo. Kwa mujibu wa mtandao mkubwa wa Showbiz, umeanika kipande hicho cha Beyonce na kueleza kuwa, staa huyo anayetamba na Albamu ya Lemonade anatarajia kupata mtoto wa pili kwa mumewe, Shawn Carter ‘Jay Z’ na hakutaka kuweka hadharani hadi atakapokaribia kujifungua.
Katika kipande hicho alichoachia mtandaoni na kufuta haraka, kinamuonesha Beyonce akiwa katika kampeni ya mavazi yake aliyoyaita jina la mtoto wake, Blue Ivy yanayotambulika kama Ivy Park. Mashabiki wake wengi wa kwenye mitandao ya kijamii ikiongozwa na Twitter wamempongeza Beyonce na ujauzito huo. Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi za ujauzito wake japo hakukuwa na picha zilizoonesha na sasa imeonekana wazi.