Kwa wapenzi wote wa ubuyu, tena ubuyu mtamu, basi hapa ndipo penyewe! Ubuyu uliotufi kia mubashara unatonya kuwa video queen aliyeuza sura kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Tunda Sebastian anadaiwa kumkosesha usingizi staa wa Manzese Music, Abdulaziz Chende ‘Dogo Janja’ kutokana na kile kinachosemekana kuwa ni mapenzi aliyonayo kwake.
KUMBE NDIYO CHANZO CHA BIFU!
Chanzo makini kilitoa ubuyu wa motomoto kuwa, Dogo Janja au Janjaro anayekimbiza na Ngoma ya Kidebe, amekuwa akiteseka kutokana na mapenzi aliyonayo kwa Tunda japokuwa waliwahi kuwa wapenzi zamani.
Inadaiwa kuwa, haijulikani Tunda alimpa nini Dogo Janja lakini ukweli ni kwamba anatamani kuwa naye tena na ndiyo chanzo cha bifu lake la mara kwa mara na mwandani wa Tunda ambaye naye ni staa wa Bongo Fleva, David Genzi ‘Young D’.
“Unaambiwa Dogo Janja hapati usingizi kwa sababu ya penzi alilonalo kwa Tunda. “Kama utakuwa unamfuatilia, amekuwa akiandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuwa, anamuomba Mungu ampe Tunda maisha marefu ili aendelee kumuona milele.
“Hata kwa marafi ki zake amekuwa akisema bado anampenda sana Tunda na ndiyo maana alimtungia wimbo huo wa Kidebe”.
“Nasikia hata video ya wimbo huo Dogo Janja alitaka acheze Tunda lakini siku ambayo walikuwa wanashuti, mwanadada huyo alipata emergency (dharura) ndipo akatafutwa mwingine’.
“Hivi karibuni ndiyo ameweka wazi kwamba huo wimbo amemwimbia Tunda, jambo ambalo lilimfurahisha sana mrembo huyo aliyeuza sura kwenye Wimbo wa Salome wa Diamond Platnumz na Rayvanny.
TUNDA FULL SURPRISE
“Lakini kwa upande wake Tunda amekuwa akitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea kuwa alikuwa hajui kama ndiye aliyeimbiwa lakini anaupenda sana wimbo huo,” alisema mtoa ubuyu wetu.
HUYU HAPA TUNDA
Baada ya kupata ubuyu huo, Wikienda lilimtafuta Tunda na mazungumzo yalikuwa hivi;
Wikienda: Mambo vipi Tunda, unaongea na Wikienda hapa.
Tunda: Karibu, niambie.
Wikienda: Kuna habari kuwa ule Wimbo wa Kidebe alioimba Dogo Janja amekuimbia wewe, unajua?
Tunda: Nimejua hivi karibuni na nimefurahi sana kiukweli maana aliniomba niwe video queen lakini ikashindikana. Siku aliyokuwa anashuti nilipata emergency, lakini kiukweli nimefurahi sana.
Wikienda: Kilichokufurahisha zaidi ni nini?
Tunda: Nimefurahi kwa sababu ni wimbo ninaoupenda sana kabla hata sijajua kaniimbia mimi.
Wikienda: Mliwahi kuwa wapenzi zamani, je, mna mpango wa kurudiana?
Tunda: Kama tutarudiana mtasikia tu, mapenzi hayajifi chi kwa hiyo wewe sikilizia.
Wikienda: Lakini kuna taarifa kwamba Dogo Janja hapati usingizi analiwewesekea penzi lako, je, unalijua hilo.
Tunda: Hahahaa…sijui ndiyo nasikia kwako maana hajaniambia.
DOGO JANJA AELEKEA DODOMA
Ili kuleta mzani wa habari hiyo, Wikienda lilimgeukia Dogo Janja ambapo baada tu ya kupokea simu alisema yupo kwenye kelele akielekea Dodoma.
Wikienda: Haloo Dogo Janja, kuna habari yako hapa.
Dogo Janja: Samahani niko kwenye kelele naelekea Dodoma mawasiliano siyo mazuri.
KUTOKA MEZA YA UBUYU
Dogo Janja amekuwa akinaswa mara kwa mara na warembo mbalimbali na sasa anadaiwa kumuwewesekea Tunda ambaye ni mpenzi wa Young D hivyo akiingilia penzi hilo ataharibu mambo, namshauri moyo wake ufanye kazi ya kusukuma damu kwa sasa na si vinginevyo.