SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 31 Januari 2017

T media news

Raia Marekani Waendelea na Maandamano Kumpinga Trump

Wengi wanasema dini isiwe sababu ya kubaguliwa

Raia nchini Marekani bado wanaendelea na maandamano ya kupinga amri ya kiutawala iliyotolewa na Rais Trump inayozuia kwa muda raia wanaotoka mataifa saba ya kiislamu kuingia nchini Marekani.

Hata hivyo, tangu hatua hiyo kutolewa, kumekuwa na mgawanyiko mkubwa miongoni mwa raia wa nchi mbalimbali huku baadhi wakiunga mkono hatua hiyo, na wengine wakiipinga vikali kwa kusema kuwa ni makosa watu kubaguliwa kutokana na imani zao za kidini.

Wakati huo huo, Kaimu mwanasheria mkuu nchini Marekani ameamuru idara ya wanasheria kutoitetea mahakamani amri hiyo.

Sally Yates, ambae aliteuliwa na Barack Obama, amesema bado hajashawishika kwamba inaruhusiwa kisheria.

Waandamanaji wanasema hatua hiyo ni kukiuka haki za binaadam

Baadhi ya wanadiplomasia wa Marekani wameandika waraka unaopinga amri hiyo, ambapo wamesema katu haitaifanya Marekani kuwa salama.

Lakini msemaji wa Rais amewajibu kwa kuwaambia, wafuate amri hiyo au waondoke.

Nae aliyekuwa Rais wa nchi hiyo Barack Obama amevunja ukimya kwa kutoa taarifa inayosema amesikitishwa na maandamano yanayoendelea nchini humo.

Trump aliagiza kuzuia waislam wa nchi saba kuingia Marekani

Msemaji wa Obama, Kevin Lewis, amesema kwamba Rais huyo mstaafu hakubaliani na fikra ya kubagua watu kutokana na imani zao za kidini.