SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 31 Januari 2017

T media news

Breaking News..Kocha wa Simba Afunguka Mazito Juu ya Hali ya Timu Yake,Awatolea Povu Mashabiki ..!!!


KOCHA Mkuu wa Simba, Joseph Omog ameshusha presha ya mashabiki wa timu hiyo kwa kuwataka kuwa watulivu kwa kuwa bado wana nafasi ya kurekebisha makosa yao na kutimiza lengo ambalo ni ubingwa.

Simba inashika nafasi ya pili nyuma ya mahasimu wao Yanga, baada ya Jumamosi kufungwa bao 1-0, na Azam FC katika mchezo wa Ligi Kuu, ya Tanzania Bara, uliopigwa Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Yanga imekamata usukani baada ya kuifunga Mwadui ya Shinyanga juzi kwa mabao 2-0 na kufikisha pointi 46 na kuiondoa Simba kileleni ambayo ina pointi 45 baada ya kipigo cha Jumamosi.

Akizungumza  Omog, ambaye amekuwa katika wakati mgumu kufuatia kipigo hicho alisema hata yeye pamoja na wachezaji wameumizwa na matokeo hayo, lakini mpira ni mchezo wa makosa na kilichobaki kwa sasa ni kujipanga upya ili kuhakikisha wanafikia malengo waliyokusudia mwishoni mwa msimu huu.

“Hakuna anayependa kufungwa au kutolewa kwenye nafasi nzuri , lakini mashabiki wanapaswa kujua Simba siyo lazima kila siku ishinde ingawa malengo yetu ni ushindi, hivyo inapotokea tumepoteza mchezo kama ilivyotokea Jumamosi tunatakiwa tukubaliane na matokeo alafu tujipange kwa mechi nyingine,” alisema Omog.

Mcameroon huyo alisema, kipindi hiki walichokuwa nacho siyo cha kutupiana lawama bali ni muda wa kuongeza mshikamano na kuisapoti timu yao kwa kuja kwa wingi uwanjani ili kuweza kushinda mechi zao na kuitoa