SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 28 Januari 2017

T media news

BREAKING NEWS : KIONGOZI WA WALINZI WA IKULU YA GAMBIA ATOROKA

Kamanda wa Polisi wa Jeshini (MP) katika ikulu ya Gambia, Luteni Nuha William Jammeh, yasemekana yupo mafichoni. Inasemekana alitoroka Gambia siku chache zilizopita. Kamanda huyu alitoa amri ya kukamatwa kwa maafisa kadhaa wa jeshi la nchi hiyo walioonekana kumpinga Rais aliyemaliza muda wake, Yahya Jammeh.

Kwa sasa Luteni Nuha Jammeh hajulikani alipo. Amekimbia mji mkuu wa Banjul na inaaminika kuwa amekimbilia nchini Senegal. Namba yake rasmi ya simu inayojulikana inaonesha kuwa yupo nchini Senegal ingawa simu yake imezimwa.

Akimzungumzia Nuha Jammeh, mtu aliyewahi kusoma nae darasa moja alisema: ” Alikuwa mkimya sana na anayependa sana dini. Ilikuwa ni rahisi sana kuzoeana naye kipindi kile. Baada ya kukutana na Yahya Jammeh, huwezi jua, kwa maana yule dikteta alikuwa na uwezo wa kugeuza watu wazuri kabisa kuwa mashetani.”