Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa wakati alipofanya mazungumzo na wafanyakazi wa kampuni hiyo,jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na Uongozi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) wakati alipotembelea kampuni hiyo, Jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (kushoto) akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya simu Tanzania (TTCL), jinsi ya mfumo wa kutoa taarifa kwa wafanyakazi unavyofanya kazi wakati alipotembelea ofisini hiyo jijini Dar es salaam.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Dkt . Kamugisha Kazaura akisoma taarifa ya utendaji kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (Hayupo pichani) wakati alipoongea na uongozi wa kampuni hiyo, jijini Dar es salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) Profesa Tolly Mbwete akifafanua jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa (hayupo pichani) wakati Waziri alipotembelea ofisi hiyo, jijini Dar es salaam.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wafanyakazi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL),Jijini Dar es salaam.
PICHA ZOTE NA BENJAMINI SAWE -MAELEZO.