CRISTIANO Ronaldo anafahamika kwa uwezo wake mkubwa katika kutikisa nyavu, akiwa mmoja wa wafungaji wakali wa muda wote katika La Liga ambayo ni Ligi Kuu ya soka nchini Hispania, pamoja na michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Lakini siyo tu ni mahiri katika kusakata kandanda, kwani rekodi zinaonesha mshambuliaji huyu wa timu ya taifa ya Ureno ni kiwembe wa ‘totoz’ maana hadi hivi majuzi, kulikuwa na wanawake 18 wanaofahamika kutoka naye, akiwemo mama wa mtoto wake (jina limefi chwa), Cristiano Ronaldo Jr, mwenye umri wa miaka mitano sasa.
Mzazi mwenzake huyo wamefi kia makubaliano kuwa asitambulike na alipewa kitita cha dola milioni kumi kufi kia muafaka huo na anapata huduma zote kutoka kwa Ronaldo. Alikuwa ni mfanyakazi wa hoteli moja jijini New York na alilala na mchezaji huyo mara moja tu, lakini akapata ujauzito.
Alilazimika kufanya vipimo vya DNA kuthibitisha kuwa ni mwanaye. Wafuatao ndiyo akinadada walioonja penzi la mwanasoka huyo mwenye utajiri wa Dola milioni 450 sawa na shilingi bilioni 900 za Kitanzania.
Huyu ndiye mwanamke wa kwanza kutangazwa katika vyombo vya habari kuwa ni mpenzi wa Ronaldo. Mwanamitindo huyu wa Ureno alikuwa na mkali huyo mwaka 2002.
Jordana Jardel – 2002
Mwaka huo huo, akiwa anaichezea Sporting Lisbon, Cristiano Ronaldo alidondokea kwa mwanamitindo Mbrazil Jordana Jardel.
Kuanzia Januari 2005 hadi Septemba 2006, Cristiano Ronaldo alikuwa na modo
wa Ureno, Merche Romero. Mwanzo, hakuna aliyekubali wala kukataa uhusiano wao, lakini Merche ndiye aliyetangaza kuvunjika kwa urafi ki wao.
Ni mrembo mwingine muigizaji na mtangazaji wa televisheni ambaye alikuwa mikononi mwa Ronaldo mwaka 2006.
Mwaka huo huo, zikasambaa habari kuwa mpachika mabao huyo nyota, alikuwa akitoka na binti aitwaye Mia Judaken, aliyekuwa na umri wa miaka 18 wakati huo, ambaye familia yao ilikuwa ni marafi ki na ile ya akina Ronaldo.
Gemma anadaiwa kuwa kahaba na mcheza fi lamu za ngono na inadhaniwa kuwa Ronaldo hakuwa akifahamu, lakini alikuwa naye mwaka 2007 na inasemwa alichajiwa pauni 2,940 (10, 584,000) kila alipohitaji kukutana naye.
Gemma Atinkson, mwanamitindo nyota Muingereza naye aliingia katika 18 za Ronaldo na uhusiano wao ukawa wenye misukosuko mingi kabla ya kutemana.
Kana kwamba haitoshi, Cristiano Ronaldo anadaiwa kutembea na mshiriki wa Shindano la Pop Idol la Ureno mwaka 2007, Luciana Abreu.
Huyu ni mrembo mwingine ambaye alishiriki mapenzi na Mreno huyo na penzi lao kuwa kivutio kikubwa katika magazeti ya udaku nchini Uingereza.
Nyota huyu wa Ureno alikuwa amealikwa katika hafla ya maajabu saba ya dunia na alikaa VIP katika ukumbi jijini London, wakati alipokutana na muigizaji maarufu wa India, Bipasha Basu. Wawili hao waliondoka muda mmoja usiku huo na picha zilizotolewa baadaye ziliwaonesha wakiwa kimahaba.
Mwaka uliofuata, Ronaldo alinasa katika anga za Nereida, modo wa Kihispania, lakini uhusiano wao haukudumu sana.
Miongoni mwa wanawake maarufu walioshiriki mapenzi na Ronaldo ni Paris Hilton, ambao walikuwa pamoja Juni 2009. Hata hivyo, hawakuwahi kutoa taarifa rasmi kama wako pamoja.
Wawili hawa walionekana pamoja katika mgahawa mmoja jijini Madrid na habari zikasambaa kuwa walikuwa katika uhusiano kuanzia Aprili 2010.
Cristiano Ronaldo na Imogen walianza uhusiano wa kimapenzi baadaye mwaka 2010, lakini miaka michache baadaye habari zikaanza kumhusisha mwanamke huyo na mwanasoka mwingine nyota wa Man United, Ryan Giggs.
Ilitaarifi wa kuwa Aprili 2013, Ronaldo alitumia usiku mmoja kuwa na mrembo huyo. Irina Shayk Mdada huyo (pichani) ndiye aliyedumu kwa muda mrefu na Cristiano Ronaldo na wengi waliamini ndiye angekuja kuwa mkewe.
Kulikuwa na habari za chini chini kuwa wawili hao walikuwa wamevalishana pete ya uchumba kisiri, lakini wakakanusha jambo hilo. Baada ya uhusiano
wa miaka mitano, wote wawili wakatangaza rasmi kuvunjika kwa penzi lao na kila mmoja alimtakia maisha mema mwenzake.
Huyu ndiye anatajwa kuwa mpenzi mpya wa hivi karibuni wa nyota huyo wa Real Madrid ambaye alianza naye Januari mwaka jana na ni mtangazaji wa televisheni.