SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 30 Julai 2016

T media news

NAMBA ZA MAGARI YA NAY WA MITEGO ZAHUSISHWA NA FREEMASON


  

Stori: BMM, Risasi Jumamosi
NAMBA za magari ya msanii wa Bongo Fleva, Emmanuel Elibariki ‘Nay Wa Mitego’, zinahusishwa na baadhi ya mashabiki wake kuwa ni za Freemason kutokana na kuwa za aina moja inayosomeka 966.

Uvumi juu ya kumhusisha Nay na taasisi hiyo inayosadikika kumuabudu Shetani zilianza kuenea kwenye mitandao ya kijamii baada ya picha za magari yake kusambaa mtandaoni, lakini alipotafutwa na safu hii ya burudani kuzungumzia tetesi hizo Nay alisema kuwa;

“Watu wanaongea vitu ambavyo hawavifahamu, mimi na Freemason wapi na wapi, hiyo namba ni namba ambayo huwa napenda kuitumia tu na kwa watu ambao wanasikiliza nyimbo zangu watakubaliana nami kuwa huwa napenda kuitaja, kiukweli haina uhusiano wowote na Freemason,” alisema Nay wa Mitego.