SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 30 Julai 2016

T media news

MBOWE AONGOZA WAOMBELEZAJI KATIKA MAZIKO YA BABA MZAZI WA DEVOTHA MINJA MBUNGE WA VITI MAALUM LEO

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa na Mbunge wa jimbo la Hai, Mhe. Freeman Mbowe leo Jumamosi 30/07/2016 ameongoza maelfu ya waombolezaji waliofika kumzika Baba wa Devotha Minja ambaye ni Mbunge wa viti maalum kupitia CHADEMA, marehemu Mathew Minja amezikwa nyumbani kwake Rauya Koteno Marangu mkoani Kilimanjaro.
Maziko hayo yamehudhuriwa pia na viongozi mbalimba.
Kati ya viongozi wengine waliohudhuria maziko hayo ni pamoja na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Arusha mjini, Mhe. Godbless Lema, Mbunge wa viti maalum Arusha mjini, Mhe. Joyce Mukya, Mbunge wa Rombo, Mhe. Joseph Selasini, Mbunge wa Karatu, Mhe. Cecilia Pareto na Mhe. Grace Kiwelo.

Akiongea kwa niaba ya Chama cha Chadema, wabunge, wanachama na kutoa salamu za rambi rambi,Mhe. Mbowe ametoa pole nyingi kwa familia ya Mzee Mathew Minja kwa msiba huo mkubwa.
"Kila mtu atakufa na kila siku kifo kikitokea tunajifunza jambo, tukikutana kwenye misiba tunakuwa wanyenyekevu, wapole, watulivu tuliojawa huzuni na hekima, lakini baada ya hapo, tunasahau na kurudia mambo yasiyo mema, unyekekevu hakuna, upole hupotea na mambo yote mazuri hupotea miongoni mwetu, ukitokea msiba mwingine tunakuwa wanyenyekevu tena, wapole, wenye huruma n.k, wanyenyekevu, wenye huruma, wapole, tuliojawa upendo ndivyo inavyotakiwa tuwe hivyo siku zote za maisha yetu, wengi tunaogopa kufa lakini kila mtu atakufa hivyo, tunavyoishi, tuishi kwa upendo siku zote, Baba yetu Mathew ametangulia lakini kesho atajui ni nani anafuata, hivyo yatupasa kupendana na kujiandaa kwa safari hiyo ya mwisho kwa kila aliye mwanadamu" amesema Mbowe.