SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 28 Julai 2016

T media news

UCHUMBA WA JACK DUSTAN WATIBUKA,KISA KIZITO CHATAJWA


METIBUKA! Ule uchumba uliodumu kwa zaidi ya miaka mitano umeingia mdudu baada mchumba wa mshikiriki wa Shindano la Maisha Plus (Season 1), Jacqueline Dustan, Hamis kuamua kuinua mikono juu na kusema sasa basi na hataki tena ndoa.

Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na wawili hao, mara nyingi Hamis alikuwa akililia kuwa na mtoto ili aweke heshima kwa wazazi lakini amekuwa akipigwa danadana na mshiriki huyo na kuambiwa kuwa muda bado na kwamba wakaekae kidogo ndiyo watafute mtoto.

 “Yaani maskini kaka wa watu hadi utamuonea huruma, kila kukicha alikuwa anadai mtoto lakini anapigwa danadana na kuambiwa kuwa muda bado kitu ambacho kilikuwa kikiusononesha sana moyo wake kama siyo kuubonyezabonyeza,” kilibonyeza chanzo hicho.

Ndugu wakomaa

Chanzo kilizidi kumwaga ubuyu bila kugeuza jicho kuwa, kutokana na mgogoro huo uliokuwa ukiendelea ndani kwa ndani bila gazeti lolote kujua, mara kadhaa Hamis alikuwa akisumbuliwa na ndugu zake kuhusiana na mtoto na aliamua kukaa chini tena na mpenzi wake huyo kujadili hilo lakini hakukuwa na mabadiliko yoyote hivyo aliamua kunawa mikono kama mbwai na iwe mbwai.

“Unajua ndugu wa Hamis hadi wazazi wake walikuwa wakimsumbua kila kukicha kuhusu suala la mtoto maana waliona uchumba wao ni wa muda mrefu usiyo na majibu yoyote ya kufurahisha familia lakini Hamis kila mara alikuwa akimtetea mpenzi wake huyo huku akijaribu kukaa naye pembeni kuzungumza na bado staa huyo alishikilia msimamo wake kuwa muda bado.

Ugumba wahu-sishwa

“Ilifika kipindi tukadhania huenda mwenzetu ni mgumba na yupo na Hamis kwa ajili ya kuponda naye raha wala siyo kumzalia. Kwa kuwa Hamis alikuwa akimpenda Jack kwa dhati na wametoka naye mbali na tena walikuwa katika mikakati ya kuoana basi tukaacha kuwaingilia,” kilipigilia msumari wa nukta chanzo hicho.

Jack huyu hapa

Amani lilipopata taarifa hizo ngumu kumeza, lilianza kuwasaka wahusika hao ili kuwauliza kama kuna ukweli juu ya madai hayo ya kuvunjika kwa uhusiano wao, huyu hapa Jack msikie;

Amani: Jack kuna tetesi uchumba wako umevunjika kisa mtoto?

Jack: Daah! Sasa hicho kweli ni kisa kinachoweza kuvunja uchumba wangu kweli, ningekuwa sizai kabisa je?

Amani: Sasa mbona inadaiwa umembania mpenzi wako kumzalia mtoto mpaka akaamua kuachana na wewe?

Jack: Si kwamba nambania, bado kuna mambo yangu binafsi namalizia ndiyo maana ishu ya mtoto nimeisubirisha kwanza na nikiyaweka sawa mbona hilo jambo dakika tu!

Amani: Inadaiwa kuwa ni kama unamzungusha jamaa ndiyo maana kaamua kusepa?

Jack: Kusepa? Hapana,  hawezi bwana, kwanza aende wapi wakati kwangu kafika, wee elewa muda ukifika nitamzalia tu wala haina shaka kabisa.

Hamis naye huyu hapa

Baada ya kuzungumza na Jack, Amani pia lilimvutia waya mchumba wa Jack, Hamis ambapo alisema kuwa ni kweli ana mgogoro na mpenzi wake huyo kuhusu mtoto.

 “Yote hayo yanayodaiwa ni kweli kabisa tuna mabishano mazito kuhusu mtoto lakini bado sijafikia uamuzi wa kuvunja uchumba maana ningetaka kuvunja, ingekuwa kipindi kile alichokuwa akinizungusha kupeleka barua ya uchumba nyumbani kwao kwa mara ya kwanza,” alisema Hamis.

Kumbe si mara ya kwanza

Tangu Jack aingie kwenye uhusiano na Hamis, imekuwa ni kawaida yake kumzungusha pindi linapotokea jambo siriazi la kifamilia, ikumbukwe pia kipindi cha nyuma alishawahi kumzungusha kwa kumpiga kalenda kupeleka barua ya posa nyumbani kwao mpaka baadhi ya ndugu wa staa huyo kuingilia kati jambo hilo ambalo lilikuja kufanikiwa.