RAIS MAGUFULI : CHADEMA MSIWAPE VIJANA VIROBA ILI WATANGULIE KWENYE MAANDAMANO,TANGULIENI NINYI VIONGOZI


Juzi Chama cha Demokrasia na maendeleo ‘CHADEMA’ kilitangaza mikakati mitatu ya kupinga ilichokiita ukandamizaji wa haki na demokrasia na kuitangaza siku ya September mosi mwaka kuwa ni siku ya maandamano nchi nzima.Jana July 29 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli alianza ziara ya siku nne katika mikoa ya Singida, Tabora, Shinyanga na Geita akitokea mkoani Dodoma, ambapo alizungumza na wananchi wa Manyoni Singida na kutoa onyo kwa watakaoanzisha maandamano.
"Wasije wakanijaribu mimi ni tofauti sana, na kama wapo watu wanawatumia wakawaeleze vizuri mimi sijaribiwi na wala sitajaribiwa, siasa nzuri wananchi wetu washibe, wapate madawa, nataka hao wanaotetea maandamano watangulie wao halafu wataona cha mtemakuni"- Alisema Rais Magufuli.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

CHOMBEZO: UTAMU WA MADAM JESCA

Simulizi; MTOTO WA BOSS WANGU

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA