SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 30 Julai 2016

T media news

Celine Dion ametoa kauli hii baada ya Kijana wa Gabon kufanya maajabu ya wimbo wake

Tayari bahati ya mtende imemwangukia kijana mdogo mwenye umri wa miaka 17  kutoka nchini Gabon baada ya mwanamuziki wa Pop kutoka Nchini Canada,  Mwanamama, Celine Dion kueleza kuwa yupo tayari kuonana na kijana huyo ilikutimiza ndoto zake katika fani ya uimbaji.

Kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Samuel,  video yake imepaata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya  kijamii hii pia ni baada ya kuchagizwa na Mwanamama huyo Nyota wa Pop, Celine Dion ambaye aliisambaza kupitia akaunti yake ambapo hadi sasa imeshaonwa na mamilioni ya watu Duniani kote huku wakiisifia na wengine wakienda mbali wakimtaka Celine Dion kumchukua kijana huyo katika kazi zake.

Katika ukurasa wake wa facebook, wa Celine Dion aliandika: “Samuel, kipaji chaki ni kikubwa sana, Kama sauti yako. Natumaini tuna nafasi ya kukutana siku moja.” Aliandika Celine Dion katika ukurasa wake wa facebook sambamba na kusamba kipande hicho cha wimbo.

Pia aliongeza kuwa: “Mimi nimeguswa na nyimbo zangu kusambaa ulimwengu mzima. Natumaini tunanafasi  ya kukutana siku moja.

Endeleza ndoto yako na siku itakuja kutimia kweli. Zaidi ni kuimba kutoka moyoni, Imba  muziki wakati wote, kwani hauna mipaka” aliandika Celine Dion

Wimbo huo ambao awali uliwahi kuimbw ana mwanadada Jennifer, Celine Dion aliweza kuvuma nao mwaka  1993.

Video ya kijana huyo wa Gabon,  Samuel kwa mara ya kwanza iliweza kuwekwa kwenye blog maarufu ya nchi hiyo kabla Celine Dion kuchapishwa tena kwenye ukurasa wake huo  wa Facebook ambao watu zaidi ya milini 2.5 wameweza kutazama hadi sasa.

Hata hivyo, Kijana huyo alizungumza na shirika la Habari la  AFP  ambapo alishangaa kuona anapata ujumbe kama huo kutoka kwa mwanamuziki huyo Nyota Duniani.

“Mimi sikutarajia kitu chochote.  Sina simu wa akaunti ya facebook.  Ila ndugu yangu aliniambia Celine Dion ametuma ujumbe kupitia video yangu. Naamini pia na mimi naweza kukutana naye siku moja.” Alieleza kijana Samuel.

Kwa sasa kijana huyo anasema anajisikia vizuri kuimba  na sasa watu wanamtambua  mitaani kote. Samuel alisema kuwa yeye alianza kuimba kwa nafsi yake katika nyakati anapokuwa mapumziko shuleni.

“Wengine hawakuweza kuamini kama na mimi nawezakuimba. Wakati walipoingia darasani, walianza kupongeza kila waliponikuta nikiimba” alieleza kijana huyo kwa Mwandishi wa BBC.