IMELDA MTEMA
STAA wa filamu Bongo, Jacqueline Steven Pentezel ‘Jack Chuz’ aliyekuwa akiishi na mumewe, Gadna Dibibi anadaiwa kuachika kwa mara ya pili.Kwa mujibu wa chanzo cha karibu na staa huyo, ndoa yao imekuwa na migogoro mara kwa mara na kwamba safari hii jamaa kamuacha jumla.“Ubuyu ulioonyooka ni kwamba, yule Jack Chuz kwa sasa ameachika na safari hii sidhani kama watarudiana tena maana jamaa kamchoka,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kunyaka ubuyu huu, Showbiz Xtra ilimvutia waya Jack ambapo alifunguka;
“Jamani, jamani! Kweli nimeamini hakuna mtu anayependa maendeleo ya mwenzake, sijaachika na haitakuja kutokea. Katika ndoa lazima kuwe na migogoro ya hapa na pale ila si kuachika, watu waache kujadili ndoa yangu,” alisema Jack.
Wawili hao walioana mwaka 2013, tangu hapo wamekuwa wakikwaruzana ambapo mwaka jana walidaiwa kumwagana na staa huyo akihama nyumbani kwake, Sinza-Mori na kuhamia hotelini.