SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumamosi, 30 Julai 2016

T media news

SAKATA LA MARTILA NA MPENZI WAKE, KAKA YAKE AINGILIA KATI

Sakata la Anthony Martial na mpenzi wake wa zamani Samantha

Hili linaweza kuwa na athari kubwa kwa Martial na mashabiki wa Manchester United wanaomba hili lisitokee na kuathiri kiwango cha mchezaji huyo pale msimu mpya utakapoanza.

Anthony Martial aligundulika kuwa na mahusiano na mwanamke mwingine. Ikumbukwe tu kwamba Samantha amezaa na Martial. Baada ya kugundua kuwa Martial ana mahusiano ya nje, kuanzia mwaka jana mpaka mwaka huu, Samantha anaendelea kumkandia Martial hasa kupitia mitandao ya kijamii.

Martial anatuhumiwa na mpenzi wake huyo wa zamani kwa kutomtunza mwanawe na kumwachia mzigo wote mpenzi wake.

Hivi karibuni ali-like post ya Zlatan Ibrahimovic ambayo ilikuwa inahusiana na suala la Martial kupokonywa jezi namba tisa na kupewa Zlatan.

Kaka yake Martial aamua kuingilia kati.

Johan (25), kaka wa Anthony Martial ambaye anacheza klabu ya Troyes France, aliamua kuposti ujumbe mrefu kwenye Instagram wenye lengo la kumtetea kaka yake juu ya sakata hilo.

“Samantha, nakubali kwamba unapitia wakati mgumu wa kuzoea maisha mapya bila ya kuwa na mdogo wangu, alkini nisingependa kusikia uwongo wako tena kwasababu unamuumiza Martial pamoja na kuchafua jina la familia yetu.

“1. Wewe haujaolewa na Anthony

“2. Wakati mnaingia kwenye mahusiano, haukumkuta Martial hana kitu, bali ulimkuta akicheza Monaco na tayari alikuwa na maisha yake mazuri tu.

“3. Anthony huwa anakupa euro 3500/ kila mwezi ili kumtunza Peyton (mtoto wao) tangu pale mlipotengana –pesa nyingi mno hizo. Hivyo kulalamika kwamba huna pesa za kumnunulia mtoto kiti na uongo uliopitiliza.

“4. Anthony anampenda sana mwanawe na anapenda kumwona kila siku. Kwa sasa ndio amekuwa baba mbaya tangu mlivyoachana lakini alikuwa baba mzuri miezi mitatu iliyopita.

“5. Unaendekeza kufanya matukio ya ajabu kwenye mitandao ya kijamii suala ambalo ni aibu kubwa. Wakati ulipokuwa na Anthony ulikuwa ukifanya hivyo?

“Anthony huwa hapendi kuongea mambo yake hadharani lakini mimi naweza kumaliza suala hili.

“Kundelea kukuangalia ukileta athari ni suala lisilovumilika na nia yako ni kuendelea kujitengezea mazingira ya kupata pesa. Mamilioni ya ndoa zimevunjika na wengi wao hawalipi hata euro 3,500 kwa wanziwao, hasa baada ya kutofunga ndoa. Nina wajibu wa kueleza ukweli na natumaini kwamba utakuwa na wasaa mzuri sasa wa kumlea vizuri Peyton.

“Najua kwamba utaumia sana baada ya ujumbe huu na uko huru sasa kuandika chochote na kujiumiza mwenyewe lakini ni muhimu sana kueleza ukweli kuliko uongo.

“Anthony siku zote atakuwa bega kwa bega na mwanawe na familia yetu

“Johan”