Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Juni, 2017

Mambo Yanayokuzuia Kupata Furaha Ya Kweli Maishani Mwako

Picha
Inaweza kuonekana ni kitu cha kawaida lakini kuwa na furaha ya kweli na ya kudumu ni kitu ambacho kinatafutwa sana na watu wengi. Ndio maana ukichunguza, harakati nyingi za kutafuta maisha zinalenga hasa kupata furaha. Hata hivyo pamoja na watu wengi kuitafuta furaha sana, lakini bado wengi pia wanaendelea kugubikwa na huzuni nikiwa na maana ni watu ambao wanaishi maisha hayana furaha sana kwa sehemu kubwa. Je, hebu tujiulize ni mambo gani ambayo yanasababisha mtu mmoja akawa na furaha au mwingine akaikosa furaha? Majibu ya maswali haya utayapata kwenye makala haya. Kikubwa fuatana nasi tuweze kujifunza pamoja. 1. Kufanya kazi usiyoipenda. Ipo asilima kubwa sana ya watu ambao wanafanya kazi ambazo mara nyingi wanakuwa hawazipendi sana. Kwa lugha rahisi wanakuwa ni watu wanafanya kazi ambazo hawazifurahii, kikubwa kwao inakuwa ni kutaka kuingiza kipato tu basi. Kama unafanya kazi ya namna hii ambayo huifurahii, lakini lengo lako ni kuingiza kipato basi elewa unabeba  moja ya k...

Jinsi Ya Kujiweka Wa Thamani Kwa Mpenzi Wako

Picha
Marafiki zangu tunaendelea na mada yetu ambayo kwa hakika imekuwa ndefu lakini yenye manufaa makubwa kwenye uhusiano wetu. Nilianza kwa kueleza kwamba yapo mambo mengi sana ambayo husababisha thamani ya mtu kushuka kwa mpenzi wake. Nilishazungumza mengi katika matoleo yaliyopita lakini leo nitaendelea na kukazia zaidi kwenye athari za kuharakisha faragha. Karibu darasani. ATHARI ZA KUHARAKISHA FARAGHA Wiki iliyopita nilifafanua zaidi matatizo ya moja kwa moja ambayo mtu anaweza kuyapata kwa kuharakisha faragha ambapo nilisema kwamba kuna suala la kuchokwa na kuonekana wa kawaida. Lingine ni kuonekana mwepesi kwenye suala la mapenzi hivyo mwanaume kuwa na mashaka kwamba hata kama akifikia uamuzi wa kukuoa unaweza kuwa mwepesi kutoa penzi kwa wengine kama ulivyofanya kwake. Tuangalie vipengele vinavyofuata. (i) Hupunguza thamani Heshima ya penzi ni kwenye ndoa. Kuna uwezekano mkubwa sana wa kushushwa thamani baada ya kutoa penzi. Wanaume wengi huanza kuwa wasumbufu (kama ni kasumb...

Zifahamu Mbinu Mbalimbali za Kumpata Mpenzi Bora Katika Mapenzi

Picha
KILA mtu anapenda kuwa na mwenza mzuri, mwenye kumfaa katika maisha yake. Hata hivyo kwa bahati mbaya ni kwamba wengi wanashindwa kupata wenza wazuri. Ziko sababu nyingi lakini kubwa ni uwezo wa mtu wa kumtambua mwingine na kujua kama ni kweli anafaa au anafaa  kuendana nae au la.Wakati wa uchumba, wengi wa watu huonekana kutumiana kadi, zawadi na mambo mengine  mbalimbali yenye lengo la kuonyesha wanapendana. Aidha, wapo ambao wanashindwa kujua namna ya kutongoza; kwa ujumla kutongoza ni uwezo wa ushawishi kwamba unamwambia mwanamke unamuhitaji na kumpenda awe wako au wakati mwingine hata mwanamke anaweza kuanza. Ndio ukweli wenyewe Sio kweli kwamba kila mwanaume anajua kutongoza. Kuna wengine hata kumsimamisha mwanamke hawezi au anaogopa. Ndio unaweza kukuta mwanamume anajikanyaga namna ya kuongea. Wapo wengine wanafikiri njia sahihi ya kutongoza ni kuhonga aidha fedha au mali nk, lakini sicho hasa wanachotaka wanawake au wanaume katika mapenzi. Maneno ya kusikia kutok...

Rammy Aopoa Kifaa Cha Gambia Baada ya AGNESS Masogange Kumtema

Picha
STAA wa filamu Bongo, Rammy Gallis amenasa kifaa kipya kutoka nchini Gambia ambaye naye ni msanii wa filamu, Princess Shyngle na kusema kuwa mwanadada huyo ndiye anayemkonga nyoyo kwa sasa japo hapendi kumuuzisha sura. Akipiga stori na Star Mix baada ya meseji za mapenzi akichati na mwanadada huyo kunaswa na paparazi wetu, msanii huyo alifunguka kuwa, yupo kwenye uhusiano na mlimbwende huyo kwa muda sasa na kwamba miongoni mwa vitu vilivyomvutia kwake ni pamoja na figa matata aliyonayo. “Nilikutana na Princess nilipoenda kufanya filamu Nigeria, kwa kuwa yeye ni Mgambia lakini makazi yake makubwa ni Nigeria, nampenda sana naamini yeye ndiye tulizo la moyo wangu, mapenzi ya Kibongo yanitue kwa sasa,” alisema.

Mwanaume Amwoa Mwanaume Mwenzake Bila Kujua

Picha
Mwanaume mmoja mkoani Mtwara amekaa na mwanaume mwenzake miezi minne bila kujua. Kwa mujibu wa maelezo mahusiano yalianza baada ya kukosea namba wakafahamiana mpaka wakafikia maamuzi ya kuoana huku akijua ni wa kike. Baada ya kufata taratibu wawili hao wakaoana lakini tatizo likaja wakati wa kujamiiana mwenzake wakawa kilasiku anasema anaumwa ikawa hivyo ndani ya miezi mitatu ndipo akaja gundua kuwa ni mwanaume mwenzake. Kuhusu mavazi anasema mwenzake huyo huvaa kama mwanamke na kupika pia anajua hata kujiremba anajiremba hali iliyo mpelekea kutogundua.

Yasome mashtaka yote 28 yanayomkabili Rais wa TFF, Jamal Malinzi

Dar es Salaam . Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi hataweza kutetea nafasi yake hiyo katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Agosti 12 mjini Dodoma. Hiyo inatokana na kushindwa kufika kwenye usaili ulioanza jana na kumalizika kesho kwa kuwa yupo rumande akikabiliwa na kesi. Mbali ya Malinzi, pia Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ aliyekuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais TFF, pia amepoteza nafasi hiyo kwa kuwa naye yupo rumande. Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi TFF, Revocatus Kuuli alisema mgombea ambaye atakosa kufika kwenye usaili katika muda huo atakuwa amejiondoa kwenye uchaguzi. Malinzi, ambaye aliingia madarakani mwaka 2013 alikuwa akitetea kiti chake ambacho kingemfanya kuwa madarakani kwa miaka mingine minne iwapo angechaguliwa. Jana, Malinzi (57), Katibu Mkuu wake, Mwesigwa Celestine (46) na Mhasibu, Nsiande Mwanga (27) walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na mashtaka mbalimbali iki...

Jeshi la Laua Majambazi wanne Kibiti usiku wa kuamkia leo

Picha
Jeshil la Polisi limeua Watu wanne wanaozaniwa kuwa ni majambazi kwenye kijiji cha Pagae , Kibiti Mkoani Pwani Taarifa iliyotolewa kwa Vyombo vya Habari na DCP Lebaratus Sabas Mkuu wa Opereshini Maalumu ya Jeshi hilo Tanzania ambapo amesema kuwa majambazi hao wameuwa jana Majira ya Usiku kwenye barabara inayotoka Pagae kuelekea Nyambunda. taarifa hiyo ya DCP Sabas inasema  kuwa Askari Polisi wakiwa doria walikutana na kikundi cha watu kinachokadiriwa kuwa na watu sita wakitokea barabara kuu ya lami wakifuata barabara hiyo inayoelekea Nyambunda kilomita 100 kutoka barabara kuu. "Watu hao walipogundua kuwa watu waliokuwa mbele yao ni Askari Polisi  walikimbia vichakani na ghafla wakaanza kuwashambulia askari kwa risasi. Askari Polisi walijibu mapigo na kuanza kupambana na watu hao. " Katika mapambano hayo askari Polisi walifanikiwa kuwajeruhi kwa risasi watu wanne katika kundi hilo la wahalifu  hao. Aidha katika mapambano hayo zilipatikana silaha mbili aina ya ...

Ripoti ya Mama aliyedai Kuibiwa mtoto Hospitalini Temeke yamfikia Waziri, atoa Neno

Picha
Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu amesema ripoti ya uchunguzi wa utata wa watoto pacha ambao mmoja anadaiwa kuibwa katika Hospitali ya Temeke imebaini kuwa, mama huyo Asma Juma alikuwa na mimba ya mtoto mmoja. Akitoa ufafanuzi wa ripoti ya uchunguzi huo, leo (Ijumaa) Mwenyekiti wa Kamati ya Uchunguzi huo, Profesa Charles Majinge amesema kuwa inawezekana kuna makosa yalitokea katika vipimo vya utrasound na kwamba hata wataalam wa hospitali ya Temeke, walifanya makosa kwa kumfanyia huduma ya upasuaji bila kumfanyia vipimo zaidi vya ultrasound. Pia Profesa Majinge alisema kuwa hapakuwa na sababu ya mama huyo, Asma Juma kuandikiwa kufanyiwa upasuaji wa dharura ingawa hakufanyiwa huduma hiyo ya dharura. Kabla ya kutoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari, Waziri Mwalimu na Profesa Majinge walikutana na familia ya Asma na kuwapatia matokeo ya ripoti, matokeo ambayo hata hivyo yamemfanya mama huyo kuangua kilio.

Bifu la Diamond na EATV...Je Dulla Ndio Chanzo au Upotoshaji?

Picha
Bifu la Diamond na EATV...Je Dulla Ndio Chanzo au Upotoshaji? "Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu" Ama kweli! "Hakuna shule ya akili" bali ufahamu wa kila mmoja kwa upana wake. Upotoshaji ni mkubwa mno juu ya Dulla Plannet Mtangazaji wa Eatv/Ea Radio na Diamond Platnumz na team nzima ya Wasafi. Ila ni kazi ngumu kuwaaminisha watu ukweli ambao tayari wao wana uongo wao kichwani. La hasha hatuwezi kuchoka kuhubiri ukweli uliopo. Ingawa yapasa "Usiseme masikioni mwa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako" ila hapana kwa hili wacha tuseme ile kweli yenye kweli ili ituweke huru. Kuzimwa kwa kusikika kwa Diamond na Team yake katika vituo hivyo ya Eatv/Ea Radio wala hapaswi kulaumiwa Dulla. Kwa maana ya uhalisia Dulla ni mwenye jina kubwa ila kiutendaji kwenye ofisi ni mtu mdogo mno, ambaye hupewa amri kama apewae mtu mwingine yoyote katika ofisi yoyote ile. Ila swala hili limekuwa likichochewa zaidi na wachambu...

CR7 na Lioneil Messi waichukua dunia kwa siku 4 na kuipeleka kwenye familia zao

Picha
Sahau kuhusu Jamal Malinzi alivyohenyeshwa pale kisutu, sahau ishu za wabongo kufikiri kwamba mtaa ni kibao lakini wiki hii macho na masikio ya wapenda soka na wanahabari duniani yalikuwa Ureno kwenye familia ya Ronaldo na Argentina kwa Lioneil Messi. Wafalme wawili wa soka la dunia Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo kwa sasa hawapo katika mashindano yoyote baada ya ligi kuisha na wanakula zao tu bata huku wakijiandaa na msimu ujao wa ligi. Kama kawaida wawili hawa nu wapinzani wakubwa ndani ya uwanja kwa miaka kadhaa mfululizo wakishindana tuzo, lakini kwa wiki hii wafalme hawa inaonekana kama ufalme wao umegeukia kwenye masuala ya kifamilia kutokana na yanayowatokea wiki hii. Juzi baada ya kuondolewa na Chile katika michuano ya kombe la mabara, mshambuliaji Crsitiano Ronaldo aliuthibitishia ulimwengu kwamba amekuwa baba tena baada ya kupata watoto mapacha na mama asiyejulikana. Ronaldo baada ya taarifa hizo mashabiki wake waliamka na kumpa pongezi nyingi na akaenda mbali zaidi ...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Ijumaa ya June 30

Picha

Katiba ya Simba inasemaje kuhusu hatma ya Aveva na Kaburu? Rage kaeleza kilakitu

Juni 29, 2017 viongozi wa juu wa klabu ya Simba Rais wa klabu Evans Aveva na makamu wake Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ walifikishwa mahakamani kujibu mashtaka yanayowakabili. Hatua hiyo imefikiwa baada ya TAKUKURU kuwashikilia viongozi hao kwa siku kadhaa, viongozi hao wamesomewa mashtaka matano yakiwemo ya kughushi nyaraka ili kujilipa deni ambapo inadaiwa waliikopesha Simba dola za Marekani 300,000 huku makosa mengine yakiwa ni ya utakatishaji pesa. Swali linakuja kwamba, inapotokea viongozi wa ngazi ya juu kama hao wa Simba kushikiliwa na mahakama jukumu la kuiongoza klabu linakuwa kwa nani? Ismail Adden Rage ametoa ufafanuzi kuhusu suala hilo kwa mujibu wa katiba ya Simba anayoifahamu yeye kama haijabadilishwa. “Katika ali kama hii viongozi wa kamati ya utendaji watakaa wajitathmini ni nani miongoni mwao ambaye ni senior anaweza akakaimu kwa uda lakini badae itabidi waitishe mkutano mkuu ili waweze kuamua lakini katiba haisemi itachukua muda gani kufanya hivyo laki...

Kisukari Ni Ugonjwa Unao Weza Kudhibitiwa Kwa Kutumia Tiba Asilia

Picha
Kisukari  ni  tatizo  la  kiafya  linalo wasumbua  na  kuwatesa  mamilioni  ya  watu  duniani. Miongoni  mwa  dalili  za  ugonjwa  wa  kisukari ni pamoja  na i. Kukojoa  mara  kwa  mara  ( Watoto kukojoa  kitandani ) ii.Kunywa maji mengi kuliko kawaida na kusikia kiu kila wakati. iii.Kuwa dhaifu, kukosa nguvu na kujisikia mchovu kila wakati. iv.Kupungua uzito  kwa  kasi  au kukonda pamoja na kwamba unakula  vizuri  tena kila  wakati  kwa  sababu  ya  kusikia  njaa kila  wakati  kunakosababishwa  na  maradhi  ya  kisukari v.Wanawake  kupatwa  na  tatizo  la kuwashwa ukeni. vi.Kupoteza  uwezo  wa Kuona  vizuri. vii.Wanaume  kupatwa  na  tatizo  la  ukosefu na / ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume...

Hatimaye Kijana Aliyedhaniwa Gaidi na Kuuwawa Kwenye ATM Kuzikwa

Picha
HATIMAYE mwili wa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Salum Almas (28), unatarajiwa kuzikwa leo ikiwa ni siku takribani ya 50 tangu kuuawa na polisi kwa tuhuma za ujambazi. Almasi ambaye alikuwa mwanafunzi wa chuo hicho Kituo cha Kompyuta (UCC), akichukua masomo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (IT), aliuawa na polisi jirani na mashine ya kutolea fedha ya kielektroniki (ATM) ya benki ya CRDB iliyopo kandoni mwa ofisi za Uhamiaji, Kurasini kwa madai ya kutaka kupora fedha. Mwili wake ulihifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH). Mjomba wa marehemu, Tulleyha Abdulrahman, aliiambia Nipashe jijini Dar es Salaam jana kuwa mwili huo ulikuwa ukifanyiwa uchunguzi Muhimbili jana, chini ya mwanasheria wa familia, ndugu, polisi, tume ya haki za binadamu na kiongozi kutoka Serikali ya Mtaa wa Kurasini ambako ndiko marehemu alikuwa akiishi. Awali, baada ya mauaji ya Salum, ndugu waligoma kuuzika mwili huo wakitaka Jeshi la Polisi l...

Mwalimu afumwa akifanya mapenzi na mwanafuzi wake darasani

Picha
Mkuu wa Wilaya ya Wanging'ombe, Mkoani Njombe, Ally Kasinge ameagiza kushikiliwa kwa Makamu Mkuu wa shule ya sekondari Wanike, iliyopo katika wilaya hiyo baada ya kukamatwa akifanya mapenzi na mwanafunzi wake darasani usiku. Kasinge ametoa agizo hilo baada ya kuwepo taarifa ya kuwepo kwa watu wanaotaka kumsaidia mwalimu huyo kuvuruga ushahidi kwa kupanga na wanafunzi wenye ushahidi huo kuongea tofauti na tukio. "Kuanzia wanafunzi walitimuliwa wahojiwe na polisi na wale wanafunzi wengine waliotajwa pia wahojiwe na polisi na mwalimu mwenyewe pia aendelee kushikiliwam huyo ambaye anatuhumiwa aendelee kushiliwa na polisi mpaka tupate majibu, kwa sababu akibaki nje ataendelea kutengeneza mazingira ya kutengeneza mtandao wa kutaka kumsaidia na kupotosha ushaidi" alisema Mkuu wa Wilaya Ally Kasinge Mbali na hilo shule ya sekondari ya Wanging'ombe pamoja na Wanike zimepandishwa hadhi na sasa zitapokea wanafunzi wa kidato cha tano, walimu wa shule hizo wameweka wazi kuwa s...

Kauli ya Waziri Mkuu kuhusu maendeleo ya vita dhidi ya dawa za kulevya

Picha
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeadhimia kupambana vilivyo dhidi ya biashara haramu ya dawa za kulevya na kuhakikisha inakuwa historia nchini. Pia ametoa wito kwa wazazi wote nchini waendelee kufuatilia nyendo za watoto ili wasijiingize kwenye mtego wa dawa za kulevya na wala wasisubiri vijana wao waanze kutumia. Ametoa kauli hiyo jana (Alhamisi, Juni 29, 2017) kwenye maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani, iliyoadhimishwa mjini Dodoma. Kufuatia hali hiyo Waziri Mkuu amesema Serikali imejidhatiti kuhakikisha kuwa uzalishaji, usambazaji na matumizi ya dawa za kulevya unadhibitiwa kikamilifu nchini. Amesema katika kutimiza azma hiyo, ambayo pia inaelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya CCM, Serikali ilifanya mabadiliko ya Sheria ya Dawa za Kulevya kwa kuanzisha chombo cha kisheria cha kupambana na biashara hiyo, ambayo imeongeza adhabu kwa wanaoshiriki. Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kuimarisha chombo hicho kinachoongoza mapambano ya ...