Taifa Stars imefuzu hatua ya robo fainali ya michuano ya Cosafa 2017 licha ya kupata sare ya kufungana goli 1-1 dhidi ya Mauritius kwenye mechi ya mwisho ya Kundi A mechi iliyochezwa kwenye uwanja wa Moruleng Stadium Afrika Kusini.
Stars imemaliza ikiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Kundi A ikiwa na pointi tano sawa na Angola (ambao walilazimishwa sare ya 0-0 na Malawi kwenye uwanja wa Royal Bafokeng) lakini Tanzania inasonga mbele kwa faida ya wastani wa magoli.