SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 29 Juni 2017

T media news

Mchezaji Donald Ngoma si wa Mchezo..Akata Mzizi wa Fitina...Yanga au Simba? Jibu Hili Hapa

Mshambuliaji wa  Yanga, Mzimbabwe Donald Ngoma ameongeza mkataba wa miaka miwili kuendelea kuitumikia timu hiyo katika Ligi Kuu Bara msimu ujao.

Kupitia kurasa rasmi za mitandao ya kijamii za timu hiyo wamethibitisha taarifa za usajili huo kwa kuandika “Donald Ngoma Raia wa Zimbabwe ni mali ya Yanga kwa mkataba wa miaka miwili.”

Ngoma ambaye alikuwa akihusishwa kujiunga wapinzani wa Yanga, Simba kabla ya kuzuka kwa taarifa za kujiunga na klabu ya Polokwane City inayoshiriki Ligi ya kuu ya Afrika Kusini ‘ ambapo alitua nchini usiku wa jana na  mchana  wa leo amesaini mkataba huo.