SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 26 Juni 2017

T media news

Ijue Ijue ratiba ya kila siku ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin

Ratiba ya kila siku ya Vladimir Putin ina mambo mengi yakiwemo saa kadhaa za kuogelea, kuchelewa kulala, kutokunywa pombe kabisa. Unataka kumfurahisha Rais wa Urusi, Vladimir Putin? Mpatie vitu viwili, mbwa mtukutu kabisa na kifungua kinywa cha mayai ya ndege wa porini aina ya tombo. Hiyo ni kwa mujibu wa wasifu wa Putin ulioandikwa mwaka 2014 na mwandishi wa jarida la Newsweek, Ben Judah aliyetumia miaka mitatu kumfanyia utafiti Rais huyo wa Urusi kwa ajili ya kitabu chake kinachoitwa, “Fragile Empire: How Russia Fell in and Out of Love with Vladimir Putin.” Rais huyu wa Urusi amekuwa akitajwa sana nchini Marekani hivi karbuni kutokana na — miongoni mwa vitu vingine — uchunguzi unaolenga kubaini kampeni za Rais wa Marekani Donald Trump, msimamo wake juu ya mgogoro nchini Syria na alichokiongea kuhusu Marekani kujitoa katika majadiliano ya hali ya hewa nchini Ufaransa. Lakini akiwa nyumbani kwake nchini Urusi, maisha yake yanakuwaje? Hii ni ratiba ya siku ya kawaida kabisa kwa Vladimir Putin:

Picha kwa hisani ya: Sputnik/Kremlin/Alexei Druzhinin

Rais Putin huwa anachelewa kuamka, anapata kifungua kinywa karibu na mchana. Mara nyingi anapenda mayai kwa muda huu na kiasi kikubwa cha uji au mayai ya ndege pori aina ya tombo na juisi. Jarida la Newsweek limeripoti kuwa vitu hivyo vinapatikana kutoka “mashamba ya rafiki yake ambaye ni kiongozi wa dini nchini Urusi anayeitwa Kirill.” Katika picha hiyo hapo juu, Rais wa Urusi, Vladimir Putin (katikati), na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev wakiwa wanakula baada ya ziara katika Ziwa Ilmen mkoani Novgorod, Urusi, Septemba 10, 2016.

 

Picha kwa hisani ya: REUTERS/Yekaterina Shtukina/RIA Novosti

Akishamaliza kula, anakunywa kahawa. Katika picha hii, Vladimir Putin na Waziri Mkuu Dmitri Medvedev wakifurahia wakati wakinywa kahawa baada ya kupata kifungua kinywa katika Ikulu ya Bocharov Ruchei iliyopo jijini Sochi, Urusi, Agosti 30, 2015.

Picha kwa hisani ya REUTERS/RIA Novosti/Pool/Alexei Druzhinin

Baada ya kahawa unafata muda wa mazoezi. Jarida la Newsweek limeripoti kuwa Putin huogelea kwa muda usiopungua saa mbili. Akiwa ndani ya maji, Putin “hufikiria na kupanga kila kitu anachotaka kufanya kuhusu nchi yake,” ameandika Judah. Wakati picha hiyo hapo juu inapigwa, Putin alikuwa Waziri Mkuu wa Urusi. Hapo alikuwa anaogelea katika ziwa mojawapo kusini mwa mkoa wa Tuva, Agosti 3, 2009.

Picha kwa hisani ya: REUTERS/Michael Klimentyev/RIA Novosti/Kremlin

Akimaliza kuogelea anaingia gym. Kwenye picha hii, Vladimir Putin (kulia) na Waziri Mkuu Dmitry Medvedev wakiwa gym katika ikulu ya Bocharov Ruchei jijini Sochi, Agosti 30, 2015.

Picha kwa hisani ya: REUTERS/Stephane De Sakutin/Pool

Putin ni mtu mwenye machaguo maalumu sana kuhusu mavazi yake, anapendelea suti za Kiton na Brioni na tai zinazotengenezwa na mbunifu wa mavazi aina ya Valentino. Kwenye picha hii iliyopigwa Mei 29, 2017, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron (kulia), na Vladimir Putin wakiwa jijini Versailles, Ufaransa.

Picha kwa hisani ya: Sputnik/Alexei Druzhinin/Kremlin via REUTERS

 Rais huyu kwa kawaida huanza kazi mchana. Kwanza, Putin hukaa mezani kwake kusoma muhtasari wa kazi zake na ripoti mbalimbali za mambo ya nje na usalama wa Taifa pamoja na vipande vya video kutoka vyombo mbalimbali vya habari vya nchini Urusi na nchi za nje. Nje ya kazi, Rais wa Urusi anapenda sana kusoma.

Picha hii ilipigwa wakati Rais Putin akishiriki mkutano kwa njia ya video kuhusu kuanzishwa kwa usambazaji wa gesi asili toka eneo la Bara nchini Urusi kwenda Kisiwa cha Crimea mwezi Disemba 27, 2016.

Picha kwa hisani ya: ALEXEY NIKOLSKY/AFP/Getty Images

Mara kadhaa, mshauri wake humwonesha Putin video za kejeli kwenye mitandao ya kijamii zinazomdhihaki yeye na serikali yake. Mbali na hilo, huwa hataki kabisa kutumia teknolojia akianza kufanya kazi. Anapendelea zaidi “mafaili mekundu na kusoma makaratasi, na simu za kizamani za enzi za vita ya Soviet” kuliko kompyuta, jarida la Newsweek limeripoti.

Katika picha hii, Rais Putin amekaa kwenye dawati alipotembelea Chuo Kikuu jijini Novosibirsk, Oktoba 22, 2008.

Picha kwa hisani ya: Mikhail Metzel\TASS via Getty Images

Rais wa Urusi ni kama “bundi” kwakuwa mara nyingi hufanya kazi mapaka usiku sana. Akili yake inatulia zaidi na hufanya kazi kwa umakini mkubwa zaidi nyakati za usiku, limeandika Newsweek. Hapa Rais Vladimir Putin akiwasili kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo Kikuu cha Siberia Machi 1, 2017.

Picha kwa hisani ya: Sputnik/Kremlin/Alexei Druzhinin/ via REUTERS

Akiwa anasafiri, ratiba ya Putin huwa ni ngumu zaidi. Popote pale atakapofikia, vitu vyote hubadilishwa, kuanzia mashuka, vitu vya bafuni mpaka mabakuli ya kuwekea matunda. Pia, Putin huwa hakubali mualiko wowote wa chakula kutoka kwa mwenyeji wake ambaye hajachunguzwa na kuthibitishwa na Usalama wa Taifa wa nchi hiyo. Kwenye picha hii, Vladimir Putin akitembelea hifadhi ya farasi ya Przewalski iliyopo nje ya jiji la Orenburg, Urusi, Oktoba 3, 2016.

Picha kwa hisani ya VLADIMIR RODIONOV/AFP/Getty Images

Gazeti kila siku nchini Uingereza la The Telegraph liliwahi kuandika kwamba Putin anapenda sana ice cream aina ya pistachio. Pia alishawahi kumpa Rais wa China, Xi Jinping zawadi ya kopo kubwa la ice cream katika mkutano wa G20 uliofanyika mwaka 2007. Hata hivyo, Jarida la Newsweek liliripoti kwamba Putin akiwa anasafiri, hataki kupewa bidhaa yoyote inayotokana na maziwa. Picha hii inamuonesha Rais Putin (kulia) na maafisa wengine katika mgahawa jijini Moscow, Machi 2, 2008.

Picha kwa hisani ya: REUTERS/Mikhail Metzel/RIA Novosti

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, muda pekee ambao Putin anakunywa kiasi kidogo sana cha pombe ni kwenye sherehe za kitaifa tu, akijaribu kuonesha taswira ya kwamba hatumii pombe au ikiwa ni mbinu yake ya kujijenga kisiasa. Kwa mujibu wa jarida la Politico, yawezekana kwa makusudi kabisa kwamba Putin anajiwekea msimamo wake kujitenga na janga la ulevi nchini Urusi ili ajitofautishe na wapinzani wake na kiongozi aliyemtangulia, Boris Yeltsin. Picha hii inamwonesha Putin na aliyekuwa Rais wa Marekani, Barack Obama walipopata chakula cha mchana katika mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa jijini New York, Septemba 28, 2015.

Picha kwa hisani ya: REUTERS/Alexei Druzhinin/RIA Novosti/Kremlin

Ratiba yake ya kazi huwa ni nyepesi kiasi inapofika mwisho wa wiki ili kumuwezesha ahudhurie madarasa yake ya lugha ya Kiingereza. Siku za Jumapili, mara nyingine huwa anakwenda kusali na kuungama. Hata hivyo, Maafisa wa Serikali ya Urusi karibu na Putin wamesema kwamba “maisha yake sio ya Kikristo kiasi hicho,” limeripoti jarida la Newsweek. Kwenye picha hii, Rais Putin anawasha mishumaa katika kanisa la Life-giving Trinity jijini Moscow, Septemba 10, 2014.

Picha kwa hisani ya: Sputnik/Kremlin via Reuters

Kila baada ya wiki kadhaa, ratiba ra Putin huwekwa wazi ili kumwezesha kufanya moja ya vitu alivyokuwa akipenda kuvifanya sana ujanani mwake: mchezo wa kwenye barafu wa hockey. Putin sio tu kwamba anakaa jukwaani kuangalia bali anacheza kwenye ligi, akipambana na timu zinazounda na walinzi wake. Kwa mujibu wa jarida la USA Today, wapinzani wa Putin na wale wanaokuwa kwenye timu moja pia kwenye michezo huwa wanamuachia nafasi kubwa ya kufanya anachojisikia kufanya. Kwenye picha hii Putin (kulia) kwenye mchezo wa hockey katika Usiku wa Ligi ya Hockey jijini Sochi, Mei 10, 2016.

Picha kwa hisani ya Alexsey Druginyn/AFP/Getty Images

Putin anapenda sana wanyama. Ana mbwa watatu, wa kwanza ni aina ya Labrador mwenye umri wa miaka 15 anayeitwa Konni, mwenhine ni aina ya Akita Inu anayeitwa Yume, na wa tatu ni aina ya Karakacha anayeitwa Buffy. Picha hii inayomuonesha Rais Putin akicheza na mbwa wake Buffy (kulia) na Yume kwenye kasri lake la Novo-Ogariovo, nje kidogo ya Moscow.

Picha kwa hisani ya Sputnik/Kremlin/Alexei Druzhinin via REUTERS

Mbwa wake aitwaye Yume alizua kisanga mwaka 2016 alipoingia kwenye chumba na kumbwekea mwandishi wa Kijapani aliyekuwa akimhoji Rais Putin. CNN iliripoti kuwa alichoamua kukifanya Rais Putin ni kumfanya mbwa huyo aina ya Akita acheze mbele ya mgeni wake huyo. Kwenye picha hii, Putin anacheza na Yume kabla ya kufanya mahojiano na kituo cha televisheni cha nchini Japan, Nippon na gazeti la Yomiuri jijiniMoscow, Disemba 7, 2016.

Picha kwa hisani ya ALEXANDER NEMENOV/AFP/Getty Images

Jarida la Newsweek linaripoti kuwa Putin hupendelea zaidi kuwa nyumbani. Anachukia sana kutembelea mitaa ya jijini Moscow, hata ikiwa ya dakika 25, na anapendelea kasri lake la Novo-Ogaryovo lililo karibu na Bahari Nyeusi zaidi ya kasri lenye ulinzi mkali la Kremlin. Katika picha hii, Rais Putin anashuka kwenye gari yake kuhudhuria sherehe ya kuweka maua kwenye kumbukumbu ya Siku ya Muungano jijini Moscow, Novemba 4, 2016.