Sahau kuhusu Jamal Malinzi alivyohenyeshwa pale kisutu, sahau ishu za wabongo kufikiri kwamba mtaa ni kibao lakini wiki hii macho na masikio ya wapenda soka na wanahabari duniani yalikuwa Ureno kwenye familia ya Ronaldo na Argentina kwa Lioneil Messi.
Wafalme wawili wa soka la dunia Lioneil Messi na Cristiano Ronaldo kwa sasa hawapo katika mashindano yoyote baada ya ligi kuisha na wanakula zao tu bata huku wakijiandaa na msimu ujao wa ligi.
Kama kawaida wawili hawa nu wapinzani wakubwa ndani ya uwanja kwa miaka kadhaa mfululizo wakishindana tuzo, lakini kwa wiki hii wafalme hawa inaonekana kama ufalme wao umegeukia kwenye masuala ya kifamilia kutokana na yanayowatokea wiki hii.
Juzi baada ya kuondolewa na Chile katika michuano ya kombe la mabara, mshambuliaji Crsitiano Ronaldo aliuthibitishia ulimwengu kwamba amekuwa baba tena baada ya kupata watoto mapacha na mama asiyejulikana.
Ronaldo baada ya taarifa hizo mashabiki wake waliamka na kumpa pongezi nyingi na akaenda mbali zaidi kwa kuamua kuweka mitandaoni picha za watoto wake hao mapacha, jambo lililowafanya mashabiki wake kuzidi kufurahia suala la Ronaldo kupata watoto wa kiume na wakike.
Usiku wa Alhamisi sasa, Lioneil Messi naye akaibuka, habari kubwa ilikuwa ni harusi yake na mpenzi wake wa siku nyingi Antonella harusi ambayo inafungwa Ijumaa ya leo nchini kwao Argentina.
Harusi ya Lioneil Messi na Antonella nayo imekuwa habari kubwa dunia nzima kwani ni kati ya tukio lililovuta sana hisia za mashabiki wa soka huku watu maarufu zaidi ya 180 wakialikwa kwenda kushuhudia tukio hilo.
Siku hizi nne matukio hata ya watoto wa Ronaldo pamoja na harusi ya Lioneil Messi yamebadilisha upepo wa habari na watu wote kuangazia macho katika familia zao.