Jana watu wengi walitarajia kuona Jamal Malinzi na Mwesigwa wakipandishwa mahakamani kusomewa mashtaka, kitu ambacho hakikutokea, Aloyce Komba wakili wa Mwesigwa na Malinzi kwa upande wake amezungumzia kilichowakuta wateja wake na haki ambazo wanastahili kuepewa kuhusiana na huu mchakato ambao unaendelea.
“Ni kweli kwamba Rais wa TFF Jamal Malinzi na Katibu Selestine Mwesigwa walitiwa nguvuni siku ya Jumanne mchana na siku hiyo hakuna lililoendelea zaidi walikuwa wamekamatwa badae majira ya usiku walipelekwa kwenye vituo vya polisi lakini walitenganishwa, mmoja alikwenda kituo kingine na mwengine alipelekwa kwenye kingine hapahapa Dar es Salaam.”
“Tupo jopo la mawakili watatu tukiongozwa na wakili msomi James Bwana, tuna wakili mwingine anaitwa Mbedule kwa hiyo jana kulikuwepo na Mbedule hadi usiku mimi na Bwana tulijiunga Jumatano asubuhi, mimi nilikuwa Kisutu nikisubiri labda wataletwa hawakuletwa nikaenda Upanga makao makuu na nimefika pale nikajua tutapata muda wa kujua nini kinaendelea.”
“Mpaka jioni hatukuambiwa wanatuhumi wanatuhumiwa na nini na kama uchunguzi tayari au watahojiwa tuweze kushirikishwa kwa hiyo wakawa bado wameshikiliwa tukajaribu tuweze kupata nafasi ya kuzungumza na mkurugenzi wa upelelezi wa TAKUKURU au mkurugenzi wa uchunguzi tukaambiwa tusubiri wapo kwenye vikao.”
“Baadae nikapata taarifa kuptia vyombo vya habari kwamba TAKUKURU wamezungumza wamesema uchunguzi unaendelea na utakapokamilika watafikishwa mahakamani, lakini sisi kama mawakili tunasema, uchunguzi unapofanyika kahi za watuhumiwa lazima zizingatiwe wana haki za familia zao, ndugu zao na watu wengine hawa ni viongozi wa taasisi kubwa, mahojiano hayajafanyika tunaambiwa vilevile waliwahi kuhojiwa siku za nyuma kwa hiyo pengine wanatumia mahojiano ya nyuma.”
“Hatujui mahojiano hayo yalihusu nini hatu kama baada ya hayo mahojiano uchunguzi ulipelekwa kwa mkurugenzi wa mashtaka ya jinai DPP ambaye badae ndiye anaruhusu mashtaka yafunguliwe au uchunguzi wa sasa ukikikamilika lazima uende kwa mkurugenzi wa mashtaka ya jinai DPP halafu aruhusu mashtaka yafanyike, muda huu wana haki ya kupewa dhamana ya TKUKURU wenyewe.”
“Hawa ni viongozi wakubwa, wanaweza kuruhusiwa waende nyumbani baade waje kuripoti, kisheria hawa ni watuhumiwa tu, TAKUKURU wasifanye kama taasisi nyingine za uchunguzi nchi hii zinazokamata watu halafu uchunguzi bade, wawe weledi zaidi na sasa hivi wanaongozwa na mtu ambaye anaweledi mkubwa sana, kamishna Lowola ana uelewa mkubwa wa uchunguzi, upelelezi na ukachero, ni mtaalam na ninaamini ana wakurugenzi weledi, unapowakamata watu uwe umewachunguza tayari.”
“Lakini kama ni style ile ya kumkamata mtu, kumuweka ndani kumdhalilisha tu halafu unasema sasa tunafanya uchunguzi nadhani sio sahihi, kwa sababu hatufahamu wamekamatwa kwa sababu gani ingawa vyombo vya habari na mitandao ya kijamii inahusisha na uchaguzi, uchunguzi unaofanyika hatujui unahusu nini lakini ulipaswa kuwa umekamilika.”
“Ilo liliwahi kufanyiwa uchunguzi na waliwahi kuhojiwa labda kama kuna mapya kuhusu hilo, mimi wakili wao nafahamu na mahojiano yao yalifika hadi wakati tukadhani wangefikishwa mahakamani, hawakufikishwa, wameamua kufanya sasa kipindi ambacho tunasema haki zao zilindwe.”