Mgombea wa chama cha National Super Alliance (NASA) nchini Kenya, Raila Odinga amewaomba wafuasi wake wasifanye mapenzi usiku wa kuamkia siku ya Uchaguzi Mkuu nchini humo.
Odinga amewataka wafuasi hao kutofanya mapenzi usiku wa tarehe 7/08/2017 ambao ndio utakuwa usiku wa kuamkia siku ya uchaguzi. Alisema kuwa hilo litafanya kila mmoja ajitokeze kupiga kura siku inayofata na kwamba wanaweza kuendelea kufanya mapenzi kwa kusherehekea baada ya kupiga kura.
“Ukiwa unaenda vitani, kufanya mapenzi ni ishara mbaya,” alisema.
“Baada ya kupiga kura, sasa mnaweza kuenjoy na kusherehekea,” aliuambia umati mkubwa wa wafuasi wake katika mkutano uliofanyika uwanja wa Bukhungu, Kakamega.
Waziri Mkuu huyo mstaafu alisema kuwa Muungano wao wa NASA utahakikisha unahesabu na kutangaza matokeo ya uchaguzi huo.
“Tutakesha kwenye vituo vyote nchini, tutahesabu kura zetu, tutatangaza tulizopata na kuzilinganisha na zile zitakazotangazwa na Tume ya Uchaguzi,” alisema Odinga.
Tazama video ya Raila Odinga akiwaambia wafuasi wake wasifanye mapenzi siku ya mkesha wa uchaguzi: