SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 27 Juni 2017

T media news

Russell Westbrook atwaa NBA MVP 2016/2017, orodha kamili ya washindi hii hapa

Ulikuwa usiku mzuri kwa mchezaji wa OKC Thunder Rusell Westbrook ambapo alichukua tuzo ya MVP wa NBA kwa mwaka 2016/2017 akiwabwaga James Harden,Le Bron James na Kawhi Leornard.

Russel ambaye wastani wake kwenye NBA ilikuwa ni points 31.8,rebound 10.7 na 10.8 assists alijikuta akitokwa na machozi pale alipopanda stejini na kuanza kutoa shukrani kwa familia yake.

Hii ni mara ya kwanza kwa mchezaji kushinda tuzo ya MVP huku timu yake ikiwa nafari ya nne au chini zaidi tangu Mosses Malone mchezaji wa  Philadelphia kuwahi kufanya hivyo mwaka 1982.

Wakati Russel akibeba tuzo hiyo, mchezaji wa timu ya Golden State Warriors Draymond Green yeye alishinda tuzo ya ulinzi (defensive player of the year) na akashinda pia assists of the year huku Malcolm Brogdon akishinda tuzo ya Rookie Of The Year.

Gwiji wa zamani wa Boston Celtics Bill Russels mchango wake katika mchezo huo bado unatambulika na katika usiku huo Russels alipewa tuzo ya Life Time Achievements Awards huku kocha wa Huston Mike D’Antoni akipewa kocha bora wa mwaka.

Klay Thompson alishinda Perfomance of The Year huku Pat Bervley wa Huston akishinda Defence of The Year, Kevin Durrant alipewa best playoff moments ambayo ilikuwa dhid ya Cavs alipofunga pointi 3 na kuipa ushindj Warriors.

Ile Dunk ya Victor Oladipos kama unaikumbuka dhidi ya Atlanta Hawks ilipewa tuzo ya Dunk Bora Ya Mwaka na All Defensive Team safari hii alikwa ni Draymond Green, Rudy Gobert, Kawhi Leornard, Chris Paul na Patrick Berverley.

Rookie First Team walikuwa ni Malcolm Brogdon, Dario Saric, Joel Embild, Buddy Hield na Willy Hernangomez , katika usiku wa tuzo hizi msanii Drake ndio aliongoza huku kukipigwa show kali kutoka kwa Nicki Minaj.