SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatano, 28 Juni 2017

T media news

Nay Wa Mitego Awachana Vibaya Young Killer, Barakah Da Prince

‘MDUNGUAJI’ bei mbaya kwenye kilinge cha Hi-hop, Emmanuel  Elibariki ‘Nay wa Mitego’ amekoleza moto bifu lake na wasanii chakaramu, Baraka Andrew ‘Da Price’ na Young Killer, ambapo pamoja na mambo mengine, amefafanua kwa kina mistari aliyowaimba kenywe wimbo wake mpya wa Moto.

Katika mahojiano maalum na Global TV Online, Nay au The True Boy ameweka wazi bila kutafuna maneno, kuwa Young Killer na Baraka  wamepoteza mweleko kwenye ramani ya muziki na kwamba kuna mahali walikosea, hivyo wajirekebishe vinginevyo watarudi Mwanza kuvua samaki.

Katika kuonesha amedhamiria kuwawashia moto, prezidaa huyo wa lebo ya Free Nation, amesema Da Prince arudi ampigie magoti prodyuza Kid Bway, kwani ndiye alimuonesha mwanga wa muziki lakini malipo ya dogo ni dharau na mateke ya punda, ndiyo chanzo cha kuporomoka kwake kimuziki.

Kuhusu Young Killer, Nay alisema ni lazima amuangukie Mona Ganstar kwani amemtoa kikazi, lakini amemlipa matusi na dharau. Nay amesema watu hao ‘wamekunja’ hivyo ni ngumu kwa wasanii hao kufika mbali kimuziki. Huku akiwakumbusha kuwa na nidhamu, kuandika mashairi na kuimba havitoshi.