Bifu la Diamond na EATV...Je Dulla Ndio Chanzo au Upotoshaji? "Enyi wajinga, fahamuni werevu, Nanyi wapumbavu, mpate moyo wa kufahamu"
Ama kweli! "Hakuna shule ya akili" bali ufahamu wa kila mmoja kwa upana wake.
Upotoshaji ni mkubwa mno juu ya Dulla Plannet Mtangazaji wa Eatv/Ea Radio na Diamond Platnumz na team nzima ya Wasafi.
Ila ni kazi ngumu kuwaaminisha watu ukweli ambao tayari wao wana uongo wao kichwani. La hasha hatuwezi kuchoka kuhubiri ukweli uliopo.
Ingawa yapasa "Usiseme masikioni mwa mpumbavu, maana atadharau hekima ya maneno yako" ila hapana kwa hili wacha tuseme ile kweli yenye kweli ili ituweke huru.
Kuzimwa kwa kusikika kwa Diamond na Team yake katika vituo hivyo ya Eatv/Ea Radio wala hapaswi kulaumiwa Dulla. Kwa maana ya uhalisia Dulla ni mwenye jina kubwa ila kiutendaji kwenye ofisi ni mtu mdogo mno, ambaye hupewa amri kama apewae mtu mwingine yoyote katika ofisi yoyote ile.
Ila swala hili limekuwa likichochewa zaidi na wachambuzi wasio na hoja waliojaa uteam na upendeleo wa upande mmoja ambao huandika bila kujua kile ambacho anaandika.
Ni wazi jaman tusishangae haya kwa maana "Mchunga peku hapendi ila hana viatu" (Ufahamu)
Uhalisia ni kwamba ni kawaida mno kwa media kuzima kupiga nyimbo za msanii yoyote. Na hii huja pale msanii anapoenda kinyume na matakwa yao media husika.
Na hata kama mtangazaji mmoja ana tatizo na msanii fulani ni ngumu kwa nyimbo kuacha kuchezwa, isipokua katika kipindi chake tu. Ila vipindi vingine vitaendelea kucheza nyimbo za msanii huyo.
Ila kama tatizo limehusisha uongozi ni lazima vipindi vyote vizime kupiga nyimbo za msanii husika. Sasa tutafakari kwa upana je!kweli dulla kwa nafasi yake ya utangazaji anaweza kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond au msanii mwingine katika Eatv/Earadio?
Nguvu ya kuaminisha mashabiki wa Diamond kuwa Dulla ni chanzo cha kuzima kupigwa kwa nyimbo za Diamond na Wasafi kwa ujumla ni kubwa. Na imani ya kuamini inaendelea kupanda.
Lakini "Mjinga husadiki kila neno"
Kimsingi haipasi hata kidogo kuendelea kumnenea Dulla lugha mbaya. Bali kutafari hoja zaidi na undani wa jambo.
Lakini kama mbwa aludiavyo matapiko yake, ndivyo mtu mjinga anavyorudia upambavu wake"
By tizneez