Maambukizi katika viungo vya uzazi vya mwanamke (PID)
Wiki hii mpenzi msomaji wangu namalizia aina za magonjwa yanayohusiana na mwanamke kupata muwasho na kutokwa na majimaji ukeni, Pelvic Inflammatory Diseases ‘PID.’ Ugonjwa huu hushambulia viungo vya ndani vyote vya uzazi vya mwanamke na kusababisha mwanamke apate maumivu chini ya kitovu na maumivu wakati wa kujamiiana kwa muda mrefu. Maambukizi katika tabaka la ndani la kizazi huitwa ‘Endometritis’, maambukizi ya mirija ya uzazi huitwa ‘Salpngitis’ na pia mwanamke anaweza kupata uvimbe ndani ya kizazi ambao unakuwa umejaa usaha uitwao ‘Tubo-ovarian abscess’ na maumivu makali ya muda mrefu ya tumbo kuanzia usawa wa kitovu kushuka chini ‘Pelvic Peritonitis’. Ugonjwa huu zaidi huenezwa kwa njia ya kujamiiana na husababishwa na bakteria ‘Neisseria Gonorrhoea’ na ‘Chlamydia Trachomatis’. Wengine wanaoweza kusababisha ni ‘Gardnella Vaginalis’, Haemophilus Influenza’, ‘Enteric gram n...