Game ya Simba na Yanga ilifanya tofauti za vyama vya kisiasa kukaa pembeni pale wanasiasa wa vyama viwili pinzani zaidi Tanzania walipokutana kwenye jukwaa moja kushuhudia mechi hiyo kwenye uwanja wa taifa.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akisalimiana na Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa
Bila kutarajia, Waziri Mkuu Mstaafu wa Tanzania Edward Lowasa ambaye aligombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA alitinga uwanjani na kukutana na wanasiasa mbalimbali wa CCM ambacho ni chama alichokihama mwaka 2015 baada ya kukitumikia kwa muda mrefu.
Mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe akisalimia mashabiki uwanja wa taifa
Lowasa aliambatana na mwenyekiti wa CHADEMA Freman Mbowe ambapo walikutana na wenzao na wapinzani wao wa kisiasa kutoka CCM kama vile Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye ambaye alikuwa mgeni rasmi kwenye Dar Derby.
Waziri Mkuu mstaafu Edward Lowasa ambaye aligombea urais mwaka 2015 kwa tiketi ya CHADEMA akisaliwa mashabiki wa soka
Kitu kikubwa hapa ni namna soka lilivyo wakutanisha wanasiasa hawa mashuhuri Tanzania na namna amani ilivyotawala huku wapinzani hao wakubwa wakiwa Bungeni wakikumbatiana wakati wanasalimiana na baadae kubadilishana mawazo wakiwa kwenye jukwaa moja.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mh. Nape Nnauye akisalimiana na Simon Msuva wakati akikagua timu