Meneja mradi wa Quality Group na katibu wake Leo mapema wamefikishwa katika Mahakama Ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu tuhuma za kukiuka amri ya afisa uhamiaji, na kujaribu kutoroka.
Washtakiwa hao wamesomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu hiyo, Cpyrian Mkeha.
Mwendesha Mashtaka, Wakili wa Uhamiaji, Method Kagoma aliwataja washtakiwa hao kuwa ni Jose Kiran Meneja Mradi na Prakash Bhatt.
Akisoma hati ya mashtaka Kagoma amedai kuwa Februari 20, mwaka huu, washtakiwa hao wakiwa raia wa India na waajiriwa wa Quality Group Ltd, walimzuia afisa wa Uhamiaji kufanya kazi zake.
Kagoma amedai kuwa, watuhumiwa hao walikataa kuripoti katika ofisi za Uhamiaji zilizopo jijini Dar Es Salaam kwa kujaribu kutoroka nchini Tanzania kwa kupitia mpaka wa Horohoro,ambao ni mpakani mwa Tanga na Mombasa,nchini Kenya.
Washtakiwa hao wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana.
Mahakama iliwataka kila mmoja kuwa na mdhamini mmoja atakayeweka dhamana ya shilingi milioni tano.
kesi hiyo itatajwa tena mahakamani hapo Machi 7 mwaka huu, kwa ajili ya usikilizwaji wa awali na washtakiwa hao kuunganishwa na wenzao 14.