Siku chache baada ya serikali kuufunga mgodi wa magunga uliopo buhemba wilayani butiama mkoani mara baada ya kuua watu wawili na kujeruhi 13, wachimbaji wengine wanne waliovamia mgodi huo katika shimo namba moja maarufu kama Long Base usiku wa kuamkia leo wanasadikiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi walipokua katika shughuli za uchimbaji wa madini kinyemela.
Mpaka sasa tayari maiti mmoja imeopolewa huku zoezi la kuopoa miili mingine mitatu linaendelea pamoja na majeruhi saba wapo hospitali.
Channel Ten ilifika katika eneo hilo na kazungumza na waokoaji pamoja na mashuhuda katika ajali hiyo na hapa wanasimulia.
Masaa machache baadae kamati ya ulinzi na usalama mkoa ikafika eneo la tukio na kuzungumza na wananchi.
Kisha agizo likatolewa na mkuu wa mkoa linataka kufungwa kabisa mgodi huo huku eneo hilo likiwekewa ulinzi na askari wa jeshi la kujenga taifa.