Zainabu Rajabu
KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Mohamed Ibrahim ‘Mo’ amesema kuwa walipata ushindi dhidi ya Yanga kutokana na jinsi walivyojituma na kusikiliza maelekezo ya kocha wao walipokuwa mapumziko.
T media ilizungumza na Mohamed Ibrahim ambaye alisema wapinzani wao walikuwa wameridhika na bao walilokuwa wanaongoza hivyo wao wakatumia nafasi hiyo kuwashambulia kwa kustukiza na kupata mabao mawili.
“Wapinzani wetu waliridhika na matokeo ya kipindi cha kwanza hivyo kipindi cha pili sisi tukaingia na maelekezo ya mwalimu, tunatarajia kupata matokeo mazuri kwenye michezo yetu ijayo hatuhitaji kupoteza hata mechi moja,” alisema Mo.
Aidha, Mo alisema kuwa timu yake ilicheza kwa kushirikiana na kujituma licha ya kuwa pungufu baada ya Bokungu kuoneshwa kadi nyekundu mapema kipindi cha pili.
“Mashabiki wa Simba watarajie ubingwa kutoka kwetu tutahakikisha tunavuja jasho kwa ajili ya mashabiki wetu ambao hawakati tamaa pale tunapokosea.”