SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumapili, 26 Februari 2017

T media news

Katibu uvccm wilaya ya ukerewe ndugu Hussein Egobano akiambatana na katibu ccm wilaya ya ukerewe comrede Abubakari Ghati wamefanya ziara katika kata ya Bukongo wilayani Ukerewe,

kwa kukutana na Halimashauri kuu ya kata ya Bukongo.

Pamoja na mambo mengine katibu ccm wilaya ya ukerewe amesisitiza upendo , mshikamano na uadirifu kwa viongozi wa chama katika kata hiyo ya Bukongo,

Katibu ccm Ukerewe amewataka wanaccm kutokuchagua viongozi wanaosubiria posho ndio wafanye kazi na badala yake amewataka viongozi wenye kujitoa kukitumikia chama ndio wachaguliwe.

Pia katibu uvccm comrede *Hussein Egobano* , amewataka viongozi wa Halmashauri kuu kuuwasaidia vijana wa ccm walioko katika maeneo yao kutimiza wajibu wao , katibu alisema nyie wazee sasa mnaelekea kuchoka kwahiyo hakikisheni kwenye maeneo yenu tunapata vijana watakaorithi mikoba yenu.

Mwisho .
Viongozi waliwashukuru wajumbe kwa mahudhurio yao mazuri na kuwataka waendelee vivyo hivyo.

*Imetolewa na*
*Ofisi ya ccm wilaya*
*Ya Ukerewe.*