SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumanne, 28 Februari 2017

T media news

Manara ame-post Instagram kuhusu Kessy kukaa benchi Yanga

Afisa habari wa habari wa klabu ya Simba Haji Manara ame-post kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu mchezaji wao wa zamani Hassan Ramadhani Kessy na hali anayopitia kwenye klabu yake mpya ya Yanga.

Manara ameandika ujumbe unaosomeka: “Unakumbuka yale maneno ya aliotudhalilisha huyo dogo? Mwambieni this is Simba na benchi ndio makazi yako ya kudumu.”

Kessy aliondoka Simba mwishoni mwa msimu uliopita huku usajili wake ukizua utata mkubwa kati ya vilabu hivyo viwili vyenye nguvu kwenye soka la Bongo.

Simba wanalalamika kwamba, Yanga ilimsajili Kessy akiwa bado anamkataba na Simba hali iliyopelekea kufungua kesi TFF ambao baadae Yanga ilitakiwa kuilipa Simba zaidi ya milioni 50 baada ya kubainika kuvunja kanuni za usajili wakati wa kumsajili mlinzi huyo wa kulia.

Tangu Kessy ajiunge na Yanga ameshindwa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Yanga kwa kumtoa Juma Abdul kwenye nafasi yake.