kabila la wala watu
Waandishi wa habari wa Uingereza waliokuwa jasiri walitembelea kisiwa hicho mwaka juzi na kufanikiwa kuwahoji watu hao kutokana na tabia yao mbaya ya kula watu. Waandishi hao walikuwa wakiongozwa na mwenyeji ambaye alikuwa amestaarabika na jina lake ni Kornelius Kembaren, huyu amekuwa akisafiri na watu wa kabila hili kwa miaka 13.
Hata hivyo, anakiri kwamba kuna wakati walikuwa wakimkaripia kwa kuleta wageni katika vijiji vya na walikuwa wakitishia kuua wageni anaowapeleka kufanya utafiti katika vijiji hivyo.
Kembaren anasema viongozi wengiu wa makabila yaw ala watu walikuwa wakiamini kwamba wazungu sio watu wa kawaida isipokuwa ni mapepo ya mizimu wachafu.
Mzee mmoja ambaye aliamua kuwa wazi alisimulia jinsi alivyokuwa akila watu tena wa jinsia zote. Mahojiano yake na mwandishi huyo yalikuwa na mtu wa kutafsiri anayejua lugha ya Karowai na mwandishi wa makala haya alifanikiwa kuona mkanda mfupi wa video na mahojiano yalikuwa hivi:
Mwandishi: Umesema umewahi kula nyama ya mtu, kweli si kweli?
Mkorowai: Ni kweli nimewahi kula.
Mwandishi: Ulishiriki kuandaa nyama hiyo ya binadamu?
Mkorowai: Hapana sikushiriki kuandaa, mimi nilikuwa mdogo.
Mwandishi: Nani aliandaa?
Mkorowai: Waliandaa wazee wa kimila enzi hizo.
Mwandishi:Ulikula nyama ya mwanamke au mwanaume?
Mkorowai: Niliwahi kula nyama ya mwanamke na mwanaume.
Mwandishi: Tamu ipi?
Mkorowai: Kwa utamu, huwezi kutofautisha.
Mwandishi: Utamu wa nyama ya binadamu inafanana na mnyama gani?
Mkorowai: Utamu wake ni kama nyama ya nguruwe.
Mwandishi: Ulikula nyama ya mtu mweusi au mzungu?
Mkorowai: Sijui kama ni mzungu au mweusi.
Licha ya kabila la Korowai ambalo pia hupatikana Indonesia, kabila linguine ambalo hula watu katika kisiwa hicho linaitwa Fore.
Hawa wako tofauti kidogo na wenzao kwani katika kabila hili pamoja na kula nyama za watu, wanawake hula ubongo na wanaume hula ngozi za watu, lakini pia hula nyama na kutafuna mifupa ya watu wanaowapika.
Watafiti wa Kiingereza kutoka The Medical Research Council’s (MRC) Prion Unit wa chuo kikuu kiitwacho University College London waliokwenda kufanya utafiti kisiwani mwaka 2015 walisema akina mama wengi ambao walikuwa wakila ubongo wa watu walikuwa wakikabiliwa na ugonjwa wa kusahau ambao kitaalamu huitwa Alzheimer. Kabila hili hupatikana mashariki mwa Papua New Guinea.
Kabila hili ambalo miaka ya 1950 walikadiriwa kufikia idadi yao kuwa ni 20,000 katika Wilaya ya Okapa na enzi hizo kabila hili lilikuwa ni vigumu kwao kukutana na makabila mengine, hasa ya duniani.
Bado kabila hili hufanya matambiko yao kwa kutumia mavufu ya vichwa na mengi ni ya wale watu waliowala na wengine katika matambiko hudiriki kulala na mafuvu hayo.
Kabila hili liliwahi kupata magonjwa ya kibinadamu kutokana na kula wenzao mwaka 1960 na ilisababisha wengi kufariki dunia kutokana na kukumbwa na magonjwa ya kuambukiza hasa ugonjwa uliokuwa ukijulikana kwa wenyeji kama ugonjwa wa kuru ambao ulikuwa ukishambulia mapafu.
Wavulana ambao hupewa jukumu la kuua mtu aliyeamuriwa kuliwa kabla ya kuidhinishwa kufanya kazi hiyo hufanywa jambo moja la kikatili sana. Je ni jambo gani hilo?
Fuatilia mkasa huu wa kusisimua hapahapa wiki ijayo.