SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Jumatatu, 27 Februari 2017

T media news

Jinsi Ya Kufanya Mambo Magumu Kuwa Rahisi

Ni rahisi kufanikisha jambo lolote, ikiwa jambo hilo utataanza kulifanya mara moja na kuacha kusubiri.

Ni rahisi kujifunza kitu kipya kwenye maisha yako, ikiwa utaamua kweli kujifunza kila siku.
Ni rahisi kutoka kwenye kushindwa, ikiwa kama utachukua jukumu la kujaribu tena na tena.

Ni rahisi kusogea hapo ulipo kimaisha, ikiwa utaweka nia na juhudi kubwa ya kutaka kutoka hapo ulipo na kwenda ngazi nyingine kimafanikio.

Ni rahisi kuwa na watu wanaokutia moyo, ikiwa wewe utaamua kuwa wa kwanza kuwatia moyo wengine kufanikiwa.

Ni rahisi kuweka akiba na kuanza kukuza utajiri, ikiwa kuanzia leo utaamua kuanza utekelezaji.
Ni rahisi kukamilisha lile jukumu ambalo linasemwa sana kwamba, haliwezekani, ikiwa wewe utaligawa jukumu hilo na kuanza kulifanyia kazi.

Ni rahisi kuongeza kipato chako, ikiwa utajifunza kuwekeza hata kama ni kidogo katika maisha yako.
Ni rahisi kuyafanya maisha yako yakawa na maana, ikiwa kila siku utachukua jukumu la kufanya mabadiliko kidogo kidogo.

Maisha yako yanaweza kuwa kama unavyotaka yawe wewe, ikiwa wewe kwanza utachukua jukumu la kuyafanya maisha yako yakawa rahisi.

Acha kufanya mambo au maisha yako yakaonekana magumu sana hasa kwa zile hali ambazo ulikuwa unaweza kuzibadili kabisa.

Kumbuka, Ni rahisi kuanza jambo jipya, ni rahisi kujaribu tena pale uliposhindwa, ni rahisi kufikiri jinsi utakavyofanya maisha yako yakawa bora zaidi, sasa jiulize ni wapi unaposhindwa?

Kwa jinsi unavyofanya kidogo kidogo kwa yale mambo yanayoonekana magumu, siku hadi siku, kuna wakati utakamilisha mambo hayo magumu na hutaweza kuamini.