Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Februari, 2016

Zijue Fursa 150 za biashara na miradi mbalimbali nchini Tanzania

Picha
1. Kununua Mashine za kukoroga zege na kukodisha. 2. Kununua Mashine za kukata vyuma na kuzikodisha. 3. Kutengeneza na kuuza tofali 4. Ufundi, Website updating/Database: Katika Halmashauri, Manispaa, Mashule, Wizara, Wilaya na Makampuni mbalimbali. 5.  Kuanzisha kituo cha redio na televisheni 6. Kufunga na kutengeneza vifaa mbalimbali vya electroniki na mawasiliano mfano; compyuta na vifaa vya compyuta na mawasiliano. 7. Kuuza software; mfano Antivirus, Operating Systems, Pastel, Tally, Myob, n.k 8. Kushona na kuuza nguo. 9. Kufungua Duka la kuuza nguo mpya; suit, socks, batiki, nguo za asili, Mashuka, Mashati, Suruali, 10. Ufugaji wa mifugo mbalimbali mfano Kondoo, Mbuzi, Ng’ombe, Kuku, Bata, na wengine. 11. Kufungua stationery, kuuza (supply) vitabu na vifaa mbalimbali ktk mashule na vyuo. 12. Kutoa ushauri mbalimbali wa Kitaalamu. 13. Kuuza viazi, mahindi, mihogo, kutengeneza popcorn na kuziuza. 14. Kusajili namba za simu na kuuza vocha 15. Kuwa na mradi wa ...

Sina Mpango wa Kuoa Mtu - Ney wa Mitego Afunguka..

Picha
Msanii Ney wa Mitego amesema kwa sasa hana mpango wa kuoa na wala hafikirii kuoa, licha ya kuwa na watoto ambao wanahitaji malezi ya mama. Ney ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kusema kwa sasa hayuko kwenye mahusiano yoyote, na suala la kuoa kwake ni suala zito, hivyo hawezi kukurupuka na kuchukua uamuzi wa kuoa. "Kusema kweli kabisa nimeulizwa swali ambalo sijaulizwa muda mrefu, na nikiulizwa huwa nalikwepaga, kufuatana na mahusiano ambayo nimekuwa nayo katikati, namshukuru Mwenyezi Mungu amenijalia watoto, for this time nikisema nizungumzie kuhusu ndoa nitadanganya, mi sifikirrii kabisa kuhusu kuoa for this time, kwa bahati mbaya au mzuri mi sipo kwenye mahusiano, sitaki kukurupuka, unajua ukifunga ndoa kwa sisi, mi ni mkristo hiyo ndo nitolee, yani hapo ndo umejicomit umeshaingia kwenye 18 ambazo huwezi kuzipangua tena, sifikirii kuoa, siwazi na sidhani kama nina huo mpango", alisema Ney wa Mitego. Pamoja na hayo Ney wa Mitego amekiri kuwa na ...

Hatimaye Rayuu Wa Bongo Movies Aolewa na Mwarabu..Mwenyewe Adai Wengi Watashangaa..

Picha
Cherekochereko! ikufikie kuwa mwigizaji wa sinema za Kibongo aliyejipatia umaarufu baada ya picha zake za utupu kuzagaa mitandaoni, Alice Bagenzi ‘Rayuu’, hatimaye ameolewa na mfanyabishara mwenye asili ya Kiarabu aitwaye Ahmedi Said. Kwa mujibu wa chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Rayuu, ndoa hiyo ilitarajiwa kufungwa kwa siri Ijumaa iliyopita nyumbani kwao, Kigogo jijini Dar bila mwaliko wa marafiki zake ili ishu isivuje. Baada ya kunyetishiwa ‘ubuyu huo’, mwanahabari wetu alikula mingo jirani na nyumbani hapo hadi cherekochereko ilipoanza ndipo akatinga ndani huku ishu hiyo ikiwa imehudhuriwa na watu wachache bila wasanii wenzake. Hata hivyo, baada ya kufanikiwa kunasa tukio hilo mwanzo hadi mwisho, Ijumaa Wikienda lilimbana Rayuu na kumuuliza kulikoni kuolewa kimyakimya tena bila wasanii wenzake wa Bongo Muvi ambapo alisema hakutaka matangazo ndiyo maana akaona bora aifanye kwa siri kwani si wote wangefurahishwa na hatua hiyo. “Sikualika ms...

MAUMIVU YA TUMBO

Picha
Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima. Maumivu Ya Tumbo Ni vizuri ukijua aina ya maumivu ya tumbo unayopata pamoja na dalili zinazoambatana nayo. Hii itasaidia kujua sababu ya maumivu na katika matibabu. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma, kuungua, kukandamiza, kukata au. Yanaweza kuwa yanakuja na kuacha baada ya muda fulani. Pia yanaweza kuambata na dalili nyingine kama kutapika, kuharisha, kukosa choo, kupata choo chenye damu, tumbo kuvimba na homa. Sababu za Maumivu ya Tumbo Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo. Maumivu chini ...

Kikwete: Nitaachia Uenyekiti wa CCM, Lakini Sitaacha Vikao vya Ndani CCM

Picha
Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho. Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete amesema kuwa ataachia nafasi hiyo hivi karibuni na kumkabidhi Rais Magufuli, lakini alitoa angalizo kuhusu uhusika wake kwenye chama hicho baada ya kujivua kofia hiyo nzito. Ingawa Katiba ya Chama hicho inaeleza kuwa mwenyekiti mpya atapatikana mwaka 2017, Mwenyekiti wa Chamo hicho, Dk. Jakaya Kikwete amepanga kuachia nafasi hiyo mapema (mwaka huu) kama ilivyokuwa kwa watangulizi wake. Akiongea jana kwenye uzinduzi wa Kitabu cha maisha ya kada maarufu wa chama hicho, Marehemu Captain John Komba, Dk. Kikwete alieleza kuwa ataachia nafasi hiyo lakini hataacha kushiriki vikao vya ndani na mambo ya maamuzi ya chama hicho. “Uenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi nitaachia, lakini mambo ya ndani yanayohusu chama hiki...

BREAKING NYUZZZZ....: MABWENI YA SHULE YA SEKONDARI IYUNGA JIJINI MBEYA YANATEKETEA KWA MOTO, CHANZO BADO HAKIJAFAHAMIKA

Picha
 Askari wa Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, akiendelea na jitihada za kuuzima moto unaoendelea kuwaka na kuteketeza Mabweni ya shule ya Sekondari Iyunga jijini humo, chanzo cha moto huo bado hakijajulikana mpaka sasa, na jitihada za kuuzima zinaendelea.  Kikosi cha Zimamoto Jijini Mbeya, kikiendelea na jitihada za kuusima moto huo. Baadhi ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Iyunga jijini Mbeya, wakiwa wakiwa nje ya Shule yao wakiangalia bila kujua cha kufanya wakati Mabweni yao yakiteketea kwa moto. Picha na habari kamili itawajia baadae kidogo.

Naibu Spika akaangwa kwa mafuta yake

Naibu Spika, Dk Tulia Ackson amesema kazi za mbunge si kupiga kelele bungeni ili aonekane kwenye luninga, bali ni ushiriki wake katika kazi za maendeleo kwenye jimbo lake. Lakini kauli hiyo imepingwa vikali na baadhi ya wabunge wa upinzani ambao wamesema ukosefu wa uzoefu ndiyo uliomfanya atamke hayo. Dk Ackson ambaye ameingia kwa mara ya kwanza kwenye chombo hicho kwa kuteuliwa na rais na baadaye kushinda uchaguzi wa naibu spika baada ya kupitishwa na CCM, alitoa kauli hiyo juzi usiku jijini Mbeya wakati wa hafla ya kumpongeza kwa kuchaguliwa kushika nafasi hiyo iliyoandaliwa na wadau wa maendeleo wa mikoa ya Mbeya na Songwe. Aliwataka wananchi kuacha kuwafurahia wabunge wanaozungumza kwenye Bunge bila kuonyesha vitendo kwenye majimbo yao. Alisema hata kama mbunge hapati fursa ya kuzungumza chochote bungeni, hilo lisiwape shida badala yake, waangalie anavyofanya kazi kwenye jimbo. “Angalieni wabunge wenu wanafanya nini majimboni ukilinganisha na kuonekana kwenye TV, na pia ...

BAD NEWS!!!

BAD NEWS!!! KWA WALE WENYE NDUGU AU JAMAA, SHULE YA IYUNGA TEC YA JIJINI MBEYA INAUNGUA SAAN YANI SAIZ NA WANAFUNZI WALIA BALAA, MOTO UMEPAMBA KARIBIA BWENI LOTE, FIRE MPAKA SAIZ BADO HAIJAFIKA!!! UKISIKIA TANGAZO ILI MJULISHE MWINGINE
Jumuiya mbalimbali zisizo za serikali zimetoa wito wa kufanyika uchunguzi kuhusu mauaji ya wanakijiji huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.Innocent Segihobe ambaye ni Katibu Mkuu wa jumuiya zisizo za serikali amesema uchunguzi huo unapaswa kuweka wazi majukumu ya kufanya baada ya mauaji ya wanakijiji cha Nyanzale katika eneo la Rusthuru huko Kivu Kaskazini, Congo DR. Segihobe amewatuhumu viongozi wa kisiasa wa eneo la Rusthuru kwamba wanahusika katika kudumisha machafuko na mapigano huko Kivu Kaskazini.Mapigano yaliyotokea baina ya wakimbizi na wakazi wa kijiji cha Rusthuru yalianza baada ya kupatikana maiti ya mkimbizi mmoja katika eneo hilo. Wakimbizi hao wanawatuhumu wanakijiji kuwa ndio waliomuua mkimbizi mwenzao.Watu watano wameripotiwa kuuawa na nyumba zaidi ya 40 kuteketezwa kwa moto katika machafuko hayo. Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Rusthuru wamekimbilia katika kambi za askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa

WATU SABA AKIWAMO MTOTO WAUWAWA KWA RISASI MAREKANI

Picha
Watu saba wameuwawa kwa kupigwa risasu akiwemo mtoto wa miaka nane huku wengine kadhaa wakijeruhiwa katika tukio la mauaji lililotokea huko Kalamazoo, Michigan nchini Marekani jana usiku.. Mkuu wa Usalama wa Umma wa Kalamazoo Jeff Hadley mtuhumiwa wa mauaji hayo amekamatwa leo asubuhi. Polisi wamesema mtuhumiwa huyo amekamatwa kwenye gari linaloshabihiana na lililotumiwa mshambuliaji, ambapo pia bunduki ilipatikana kwenye gari hilo. Mtuhumiwa huyo mzungu mwanaume mwenye umri wa miaka 45, ni mkazi wa kaunti ya Kalamazoo, imeelezwa alijisalimisha bila ya purukushani.

MH. MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA KUCHAKATA GESI, MADIMBA-MTWARA

Picha
 Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa (MB) mwishoni mwa juma alifanya ziara katika mitambo ya kuchakata gesi asilia iliyopo Madimba, Mtwara. Katika ziara hiyo, Mh. Majaliwa aliweza kujionea uwekezaji wa kimataifa uliofanywa na Serikali kupitia Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanznaia (TPDC). Akiongea wakati wa ziara hiyo, Mh. Majaliwa alisema “nawapongeza sana kwa kazi nzuri mnayoifanya, ni jambo la fahari kuona Watanzania wakiendesha mitambo hii tena kwa umakini mkubwa”. Akiwa kiwandani hapo, Mh. Majaliwa aliweza kuzungumza na watumishi wa TPDC na kuwataka kuendelea kuchapa kazi kwa kutumia utaalam wao na kutambua kwamba Taifa linawategemea katika utendaji wao. Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa TPDC, Dkt. James Mataragio alieleza juhudi za TPDC kuuelimisha umma kuhusu sekta ndogo ya gesi na mafuta ili kuwaandaa wananchi na fursa zilizopo na zinazokuja na miradi mikubwa ya gesi.  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano w...

IBRAHIM AJIB AKABIDHIWA TUNZO YA MCHEZAJI BORA

Picha
Katika kuongeza morali na kuwazawadia wachezaji wanaofanya vizuri, Klabu ya Simba ilianzisha Tunzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi kuanzia mwezi wa Septemba 2015. Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na huduma ya Simba News.Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana ka...

Utani wa mpira wasababisha kifo cha mwanafunzi

Mwanafunzi wa kidato cha tatu katika Shule ya Sekondari ya Kinyara wilayani Rungwe Mkoa wa Mbeya, Deogratius Mwanangwa amefariki dunia  kwa madai ya kusukumwa na mwanafunzi mwenzake na kuanguka kutoka kwenye kitanda cha juu ‘deka.’ Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Ahmed Msangi alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku wakiwa bwenini. Alisema wanafunzi hao walikuwa wakibishana kuhusu Simba na Yanga. Msangi alisema Mwanangwa aliwahishwa Hospitali ya Igogwe kwa matibabu lakini alifariki dunia. Mganga Mkuu wa hospitali hiyo, Oyeti Mwakosya alisema mwanafunzi huyo alifikishwa hospitali akiwa amepoteza maisha. Dk Mwakosya alisema uchunguzi ulibaini kuwa kifo chake kilitokana na mtikisiko wa ubongo.

Mbowe aonya utumbuaji majipu

Picha
Mwenyekiti wa Chadema ambaye pia ni mwenyekiti mwenza wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), amekemea kile alichokiita “fukuza fukuza” ya watumishi wa umma bila kufuata taratibu. Kauli ya Mbowe imekuja wakati Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Rais John Magufuli, ikiwa katika kampeni ya kufukuza na kusimamisha watumishi wa umma wanaotuhumiwa kuhusika katika ubadhirifu, wizi, uzembe na njama za kuhujumu mapato. Operesheni hiyo inafanyika kwa kuwasimamisha kazi watumishi hao huku uchunguzi ukiagizwa kufanywa wakati tuhuma zao zikiwa zimeshatajwa hadharani. Tayari watumishi zaidi ya 160 wameshasimamishwa au kufukuzwa kazi tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani. Kati yao, tayari wachache wamefikishwa mahakamani. Mbowe alisema ufukuzaji watumishi wa umma bila ya kufuata taratibu hautakiwi na kuwataka viongozi wa dini kukemea mwenendo huo. Alitoa kauli hiyo mbele ya Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Fredrick Shoo katika ibada maalumu ili...

BREAKING NEWS : KIONGOZI WA MAJAMBAZI WANAOVAMIA MABENKI TZ HUYU HAPA

Picha
Siku nne baada ya majambazi 12 kuvamia Benki ya Access tawi la Mbagala, jijini Dar es Salaam na kuiba Sh. milioni 20 na kusababisha vifo vya watu sita, mtu anayedaiwa kuwa kinara wa uhalifu huo ametiwa mbaroni baada ya kutajwa na washirika wake, akiwamo aliyekamatwa  akiwa anafunga ndoa. Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili ilizipata zinaeleza kuwa, kinara wa ujambazi huo alikamatiwa Sinza Mori, wilaya ya Kinondoni jana, saa 11:00 jioni. Kwa mujibu wa taarifa ambazo Nipashe ilizipata, kikosi kinachoshirikisha askari wa majeshi mbalimbali ikiwamo, polisi na la wananchi wa Tanzania, kilinasa watu wanne kwenye sherehe ya harusi baada ya kufuatilia mawasiliano yao ya simu.  “Unajua sasa hivi hili suala linahusisha jeshi ambao wamefuatilia kwenye mtandao na kunasa simu za watu wanne ambao wamekamatwa huko Mbagala, akiwamo bwana harusi na watu wengine wanne,” kilisema chanzo chetu.Taarifa hizo zinasema baada ya watu hao kukamatiwa wakiwa wanafunga ndoa msikitini, wa...

Siri ya ujambazi Dar bayana

Picha
Wadau mbalimbali wakiwamo wananchi, polisi, Jeshi la Wananchi (JWTZ), Wizara ya Mambo ya Ndani wamezungumzia kuongezeka kwa ujambazi katika jiji la Dar es Salaam. Baadhi wamesema matukio hayo ya ujambazi yamesababishwa na udhaifu wa Jeshi la Polisi katika kukabiliana na wahalifu wanaotumia silaha kupora fedha kwenye mabenki na maduka makubwa. Sababu nyingine zinazotajwa ni majambazi hao kuhukumiwa vifungo vya muda mfupi na kutoka gerezani mapema, hali inayorudisha nyuma juhudi za Serikali kupambana na uhalifu. Kadhalika, umbali wa kituo kimoja cha polisi mpaka kingine, na mara nyingine baadhi kufungwa siku za mwisho wa juma, ni moja ya mambo yanayosababisha kuongezeka kwa uhalifu. Chanzo kingine kilichotajwa kuchochea ongezeko la uhalifu ni kuhujumiwa kwa Jeshi la Polisi na baadhi ya askari wake ambao ama hutoa silaha kwa wahalifu au kushiriki. Maoni ya wananchi Mkazi wa Tandika, Iddi Shomvi alidai jana kuwa majambazi wengi wanaopora fedha kwenye mabenki ni askari wa JWTZ), wali...

Nigeria ina wafanyakazi hewa 24,000

Picha
 Serikali ya Nigeria imeondoa karibu wafanyikazi 24,000 kutoka kwa orodha ya malipo ya wafanyikazi wa umma baada ya uchunguzi kugundua kwamba majina hayo yalikuwa ghushi. Wizara ya fedha imesema hatua hii imesaidia kuokoa kima cha dola bilioni 11.5. Hii ni moja wapo ya kampeni ya kupambana na ufisadi aliyo ahidi Rais Muhammadu Buhari alipochukua mamlaka mwaka uliopita. Ufisadi na usimamizi mbaya wa fedha za umma zimetajwa kama vizingiti vikubwa dhidi ya ukuaji wa Nigeria, ambapo serikali imelazimika kubana matumizi kutokana na tisho la mdororo wa uchumi. Nigeria ndiyo yenye uchumi mkubwa zaidi Barani Afrika na pia inaongoza katika uzalishaji wa mafuta imekumbwa na matatizo ya kifedha hususan kutokana na kuanguka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia. Nchi hiyo pia inakumbwa na mfumuko wa bei, kuanguka kwa soko la hisa huku uchumi huo ukiwa na ukuaji wa chini zaidi kuwahi kutokea kwa zaidi ya muongo mmoja.

MAGAZETI YA LEO JUMATATU TAREHE 29.012016

Picha

BAADA YA UCHAGUZI KUMALIZIKA, HUU NDIYO MSIMAMO WA TFF KUHUSU RAIS MPYA WA FIFA

Picha
Shirikisho la soka barani Afrika CAF lilitoa tamko kabla ya uchaguzi wa rais wa FIFA kwamba, Afrika pamoja na vyama vyake vya soka vitamuunga mkono Sheikh Salman katika kinyang’anyiro hicho kilichofanyika February 26, 2016. Mbali na CAF kutoa agizo kwa vyama vyake vya soka kumuunga mkono Sheikh Salman bado mgombea huyo alishindwa kufurukuta mbele ya Gianni Infantino ambaye alishinda kiti hicho cha urais kwa tofauti kubwa ya kura na kuashiria huenda kuna nchi wanachama wa CAF hawakumchagua Sheikh Salmani. Shaffihdauda.co.tz imefanya mahojiano maalumu na rais wa TFF Bw. Jamal Malinzi kutaka kujua hasa ni kitu gani kimemuangusha Sheikh Salman licha ya Afrika bara lenye kura nyingi kutangaza kumuunga mkono rais huyo wa shirikisho la soka la Asia. “Tumepata rais mpya wa FIFA sasa Gianni Infantino nimeongea na waandishi wa habari wa kimataifa na sasa naongea na Clouds TV, Clouds FM na shaffihdauda.co.tz ni kwamba tumekubali matokeo ya uchaguzi, uchaguzi ni uchaguzi kikubwa sas...

Al Shabab yawaua 24 wakitizama Man U-Arsenal

Picha
 Watu 24 wameuawa mjini Baidoa Kusini mwa Somalia wakitizama mechi baina ya Manchester United na Arsenal baada ya shambulizi lililotekelezwa na Al Shabab. Taarifa za awali zinaeleza kuwa milipuko miwili mikubwa ilitokea, katika mkahawa huo uliokuwa umejaa mashabiki wa mechi kati ya Manchester United na Arsenal. Miongoni mwa wale waliouawa ni pamoja na afisa wa serikali ya jiji hilo. Mji wa Baidoa ulitekwa na wapiganaji waislamu wa Al-Shabaab mwaka wa 2008, lakini walitimuliwa mwaka 2012. Mji huo ulioko takriban kilomita 200 kutoka mji mkuu Mogadishu ni mji wa hivi punde zaidi kushambuliwa na wanamgambo hao wa kiislamu. Shambulizi la kwanza lilitokea katika mgahawa maarufu unaopendwa na wageni na viongozi wa kisiasa ambao ulishambuliwa kwa gari lililokuwa limetegwa bomu. Walionusurika waliokolewa na wanajeshi wa muungano wa Afrika AMISOM. Shambulizi hili limetokea muda mchache tu baada ya kukamilika kwa warsha ya viongozi wa mataifa yanayochangia wanajeshi wake katika jeshi ...

Atiwa mbaroni Algeria kwa mashambulio ya Paris

Maafisa usalama wa Algeria wametangaza habari ya kutiwa mbaroni raia mmoja wa nchi hiyo aliyekuwa anaishi nchini Ubelgiji kwa tuhuma za kuhusika katika mashambulizi ya mjini Paris Ufaransa.Shirika la habari la Algeria limetangaza leo Jumapili kuwa, mtuhumiwa huyo ambaye alitiwa mbaroni Jumanne iliyopita, alikamatwa mashariki mwa Algeria.Hata hivyo mwendesha mashtaka mkuu wa Algeria hakutoa wasifu wa mtuhumiwa huyo, lakini amesema, ametiwa mbaroni kwa kuhusika na shambulio la kigaidi la mwezi Novemba mwaka jana mjini Paris na kuwa na uhusiano na kundi moja la kigaidi lililoko nje ya Algeria.Kwa upande wake, gazeti la Le Soir la Algeria limelinukuu shirika la habari la Ufaransa likisema kuwa, mtuhumiwa huyo anajulikana kwa jina la Zahir Mahdawi mwenye umri wa miaka 26 ambaye aliondoka Algeria mwaka 2012 na kuelekea nchini Uturuki.Itakumbukwa kuwa, watu 130 waliuawa na mamia ya wengine kujeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufanya mashambulizi katika maeneo tofauti ya Paris, mji mkuu wa ...

Nyota ya Mbwana Samatta Yaanza Kung'aaa Ubelgiji Aipatia Timu yake Goli la Ushindi Jioni Hii

Picha
Nyota ya Samatta imeanza kuonekana Baada ya leo kuipatia timu yake ya Genk bao lililowapa ushindi dhidi ya timu ya Brugge, Akiingia kutoka Benchi Dakika ya 77 wakati matokeo yakiwa mbili kwa mbili dakika ya 81 Mbwana Sammatta alipachika bao la Tatu kwa Genk ambapo matokeo yalibaki hivyo mpaka mpira unaisha dakika ya Tisini Genk 3 Brugger 2, Brugge ndio timu inayoongoza ligi hiyo kwa sasa Visit website

Ameanga dunia Mwongozaji filamu (director) aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 63.

Picha
انا لله وانا اليه راجعون Farajullah Salahshur, mwongozaji filamu (director)maarufu wa Kiirani aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 63. Allah amrehemu, amlaze mahala pema peponi na amfufue pamoja na Mitume wake watukufu, amin. Salahshur alikuwa tayari amesha andika pia kisa cha filamu ya Maisha ya Nabii Musa AS; na uchukuaji filamu wake  ulikuwa uanze miezi michache iliyopita lakini mauti hayakumpa fursa ya kukamilisha kazi hiyo ya kheri. Inshaa Allah Mola amlipe thawabu ya amali hiyo tukufu kwa nia yake, amin.

Farajullah Salahshur, mwongozaji filamu (director)maarufu wa Kiirani aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as)

Picha
انا لله وانا اليه راجعون Farajullah Salahshur, mwongozaji filamu (director)maarufu wa Kiirani aliyetengeneza filamu za Kisa cha As-habul Kahf na Kisa cha Maisha ya Nabii Yusuf (as) ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 63. Allah amrehemu, amlaze mahala pema peponi na amfufue pamoja na Mitume wake watukufu, amin. Salahshur alikuwa tayari amesha andika pia kisa cha filamu ya Maisha ya Nabii Musa AS; na uchukuaji filamu wake  ulikuwa uanze miezi michache iliyopita lakini mauti hayakumpa fursa ya kukamilisha kazi hiyo ya kheri. Inshaa Allah Mola amlipe thawabu ya amali hiyo tukufu kwa nia yake, amin.

Tatizo la Kunuka Kikwapa, tiba hii hapa

Picha
Tatizo la Kunuka Kikwapa, tiba hii hapa Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo la kikwapa husababishwa na bakteria wanaovutiwa na jasho au unyevunyevu  chini ya kwapa. Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu inayokuwa kero kwako na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yako. Ili kwapa lako liwe na harufu nzuri, kavu na safi fanya yafuatayo Paka kipande cha limao kwenye kwapa na kuacha lipate hewa  safi ili kuua vijidudu na kutoa tezi za jasho kuondoa harufu mbaya Vaa nguo safi zenye nyuzinyuzi za asili kama pamba, hariri na sufu zitasaidia kufyonza unyevu na kuliacha kwapa lako kavu, safi na bila harufu mbaya Oga kila siku na safisha nguo kwa maji safi itasaidia kuua bakteria na ambao husababisha harufu mbaya Kunywa maji mengi kila siku yatakusaidia kutoa sumu mwilini na hivyo kupunguza harufu mbaya ya kwapa. Osha kwapa mara kwa mara kwa kutumia sabuni zenye dawa (medicated s...