Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Desemba, 2016

HUYU Hapa Ndio Mfugaji Aliyemchoma Mkuki wa Mdomoni Mkulima....Atiwa Mbaroni

Picha
Wafugaji wa kijiji cha Changalawe kata ya Masanze wilaya Kilosa mkoani Morogoro walioyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa na jeshi la polisi kufuatia tukio la mkulima Agustino Mtitu kuchomwa mkuki mdomoni na kutokea shingoni hatimaye wamerejea makazini kwao huku wakilalamikia baadhi ya mifugo yao kukatwa mapanga na watu wasiojulikana. Wakizungumza baada ya kurejea kutoka porini walikojificha kwa siku tano wafugaji hao wanawake kwa wanaume pamoja na watoto wamesema mtuhumiwa wa kosa la kumchoma mkuki mkulima wamemkabidhi kwenye mamlaka husika na hivyo wameliomba jeshi hilo kuwaacha huru wale wasiokuwa na hatia. Akithibitisha kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Ulrich Matei amesema hawatasita kuwakamata wafugaji wote wanaoendelea kusababisha uvunjifu wa amani katika wilya ya Kilosa. Nao baadhi ya wakulima wamesema kijiji hicho kimekumbwa na hofu kubwa na kwamba familia ya ndugu Mtitu aliyechomwa mkuki nayo ilitoweka na kuomba hifadhi kwa wasamaria wema....

Habari ya kusikitisha kuhusu mchezaji wa Simba kufiwa na watoto watatu

Picha
Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya msiba wa watoto wa mchezaji wetu Juuko Murshid vilivyotokea leo huko kwao nchini Uganda. Vifo vya watoto hao watatu vimekuja katika kipindi hiki ambapo mchezaji wetu huyo wa kimataifa, akiwa kwenye maandalizi ya fainali za mashindano ya Afcon, yanayotarajia  kuanza katikati ya mwezi ujao. Tunajua uzito wa kufiwa na watoto hao, na tunatambua uchungu alionao nyota wetu huyo, yeye pamoja na mkewe, lakini tunaamini Mungu atawapa subira na uvumilivu mkubwa katika kipindi hiki kigumu wanachopitia. Mwisho klabu inawatakia Wanasimba na Watanzania wote heri ya mwaka mpya 2017. Imetolewa na. *Haji S Manara* Mkuu wa Habari wa Simba SC.

Waziri Mwigulu Nchemba aguswa na hali ya Chid Benz

Picha
Hivi karibuni zilisambaa picha kwenye mitandao ya kijamii zikimuonyesha msanii wa Bongofleva Rashid Makwilo ‘Chid Benz’ akionekana kurudi kwenye dawa za kulevya. Leo December 31 2016 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amekutana na kufanya mazungumzo na mama wa Chid Benz, baada ya kuonana na mama yake Chid Benz haya ni maneno aliyoyaandika kwenye ukurasa wake wa Instagram…….. Nimekutana na kufanya mazungumzo na mama wa msanii Rashid Makwilo “Chid Benz” ambaye kwasasa amepatwa na tatizo la Dawa za kulevya. Inasikitisha na haivumiliki kuona nguvu kazi ya Taifa inapotea huku wauzaji wakinufaika kwa pesa haramu. Ifahamike wazi vita ya serikali dhidi ya magenge, wauzaji na wasambazaji wa madawa ya kulevya imeongezeka hasa katika awamu hii ya tano chini ya Mh.Rais J.P.Magufuli,hivyo anayejihusisha kwa namna yoyote ni vema akaamua kuachana nayo kabla hajakutwa na mkono wa dola. Mbali ya vyanzo vya taarifa tulivyonavyo, ni wajibu wa kila al...

BONDIA FRANCIS CHEKA AGOMA KUFUNGIWA MASUMBWI

Picha
Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania (TPBC) chini ya Rais wake, Chaulembo Palasa imemfungia kwa miaka miwili bondia Francis Cheka ‘SMG’ kushiriki mchezo huo pia imempiga faini ya Sh 500,000 adhabu ambazo Cheka amegoma kuzitambua TPBC imemfungia Cheka baada ya kugomea pambano lake dhidi ya Abdallah Pazi ‘Dullah Mbabe’ ambalo lilipangwa kufanyika Desemba 25, mwaka huu kwenye Ukumbi wa PTA jijini Dar es Salaam.  Katibu Msaidizi wa TPBC, Michael Chatta amesema kamati ya utendaji iliyokaa Desemba 27, mwaka huu imeamua kumfungia Cheka baada ya kukutwa na makosa ya kimakubaliano na promota wake. Chatta alisema kamisheni hiyo ilipokea mkataba wa promota Kaike ukimhusisha Cheka kwa ajili ya pambano lake dhidi Dullah Mbabe huku kukiwa na makubaliano ya kimkataba  kwamba anatakiwa kulipwa sh. milioni tatu za awali na shilingi milioni sita baada ya pambano hilo lakini hata hivyo bondia huyo aligomea. “Kamisheni tumeamua kuchukua hatua ya kumfungia...

PICHA 3 ZA MFALME MPYA WA THAILAND ZAITIKISA DUNIA NZIMA ONA MWENYEWE HAPA LIVE!!

Picha
Baada ya Mfalme wa Thailand kufariki Dunia mtoto wa Mfalme huyo ajulikanae kama *Maha* mwenye umri wa miaka 64 pichani akiwa na hawara yake ndiye anayetarajiwa kumrithi Baba yake, kama Mfalme mtarajiwa wa Thailand.

AISEE HUWEZI AMINI HII HAPA NDIO ORODHA YA WAIGIZAJI WA KIKE AFRIKA WENYE UWEZO KISANAA NA MVUTO WA PEKEE

Picha
10. Rita Dominic   9. Stephanie Okereke   8. Ini Edo   7. Nadi Buari   6. Jackline Appiah   5. Genevieve Nnaji   4. Jackline Wolper   3. Yvonne Okoro   2. Omotola Jalade   1. Elizabeth Michael Lulu

WAZIRI NAPE ADAI BASATA WANAONANA NA WASANII WAKATI WA KUFUNGIA NYIMBO ZAO

Picha
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Moses Nnauye amekiri kuwepo kwa udhaifu katika sheria ambazo zinaliongoza Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) lililopewa dhamana ya kusimamia na stawisha shughuli za sanaa nchini. Waziri Nape amedai kwa sasa baraza hilo linakutana na wasanii wakati wa kuzifungia kazi zao pale wanapokiuka maadili ya kazi za sanaa. “BASATA ambalo ndio baraza lipo chini yangu sio rafiki kwa msanii,” Waziri Nape alikiambia kipindi cha XXL cha Clouds FM. “Msanii anakutana na BASATA unapotakiwa kufungiwa wimbo wake au anapotakiwa kuonywa kwa kupewa adhabu. Nataka sheria ilifikishe sehemu BASATA awe walezi wa msanii. Sasa hivi wakiamua kuwa walezi akina Mngereza na wenzake ni kwa mapenzi yao. Lakini nataka sheria iwalazishe wao sio polisi, wao ni wazazi wanaotakiwa kulea na kuendeleza,” Aliongeza, “Hata Bodi ya filamu wasionekane tu wakati wakufungiana, waonekane pia wakati msanii anaanza kukua mpaka anafika mbali zaidi. Kwa hiyo ...

MSANII HARMONIZE ASEMA WCB HAKUNA CHUKI WALA MAJUNGU KATI YAO

Picha
Harmonize amedai kuwa hakuna ushindani ndani ya lebo ya WCB wala chuki tofauti na watu wengine wanavyodhania. Hitmaker huyo wa Matatizo, amekiambia kipindi cha FNL cha EATV kuwa ndani ya lebo yao hawajawahi kushindana wala wanapotoa nyimbo hawatoi kwa mashindano kati yao ila mashabiki ndio wanaowachukulia hivyo lakini kibiashara kwao inakuwa vizuri. Muimbaji huyo ameongeza kuwa hakuna msanii wa lebo hiyo anachukia pindi mwingine anapofanya kolabo na msanii mwingine mkubwa kwa kuwa kila mtu anakuwa na riziki yake na mafanikio ya mmoja ndio yakwao waote. Pia Harmonize amesema kuwa si kweli kama inavyodaiwa na baadhi ya watu kuwa wanaachia nyimbo zao kwa ajili ya kuzizima nyimbo za wasanii wengine na kuda kuwa wao wamepeana muda na kila mtu ana muda wake waliopeana kuachia nyimbo zao.

SERIKALI YAPIGA MARUFUKU TAASISI YOYOTE KUTOA TAARIFA YA FARU JOHN

Picha
Serikali imepiga marufuku taasisi yoyote ya serikali kutoa taarifa inayohusu sakata la Faru John kwakuwa suala hilo lipo chini ya ofisi ya waziri mkuu na imeshaundiwa timu ya wataalam kulifuatilia hadi serikali itakapotoa taarifa. Akiwa katika ziara ya siku mbili ya kikazi mji mdogo wa Loliondo wilayani Ngorongoro,Naibu waziri wa maliasili na utalii Ramo Makane amesema kumekuwa na mijadala inayoendelea kuhusu faru John na mengine imekuwa ikipotosha ukweli hivyo hakuna mtendaji au taasisi ya serikali itakayoruhusiwa kutoa taarifa hiyo na kusema kuwa suala hilo liko chini ya waziri mkuu. “Lakini utaratibu wa kawaida wa kufanya kazi za serikali anayeagiza ripoti ndiyo mwenye ripoti, ripoti hii ya uchunguzi ni ya waziri mkuu, atakayeweza kuitoa ripoti hii nje ni waziri mkuu, hakuna mamlaka nyingine yeyote ya serikali chini ya waziri mkuu yenye uhalali wa kutoa tamko au kutoa ufafanuzi wa jambo hili,” alisema Makane. BY: EMMY MWAIPOPO

SIMULIZI FUPI: UCHI WANGU UMENIPONZA

Picha
NIKAJIWEKA katika kundi la warembo wasioshikika baada ya wanaume kadhaa kunisifia kuwa mimi ni mrembo haswa!! Shilingi zao zikazidi kunipanda kichwani na kunifanya niwe na kiburi ambacho sikujua kama ni kiburi hadi mama yangu aliponiweka kitako na kunitamkia wazi kuwa hapendezwi na tabia zangu. Amini! Sikujua kama nimebadilika na kuwa na tabia mbovu, ningeziona vipi kama nilikuwa nazipenda na marafiki wananisifu kila wakati?? Waalimu walikuwa wa kwanza kuniwania, mkuu wa shule akafanikiwa na hatimaye akaitoa bikra yangu nikiwa kidato cha pili tu! Matokeo yangu yakawashangaza wazazi wangu, usiku sisomi lakini matokeo yangu yalikuwa mazuri.  Uchi wangu uliyaleta matokeo haya, mkuu wa shule alinipa ahadi hii kuwa nitakuwa nafanya vizuri katika masomo yangu yote.  Ilikuwa shule binafsi bila shaka waalimu walitii alichowaamuru. Hatimaye akanijaza mimba, sikujua kama ni mimba hadi dada mkuu aliponivuta kando na kunieleza kuwa nina kila dalili ya mimba. Nikamwendea mkuu wa s...

KUELEKEA CCM MPYA YA DHANA YA MABADILIKO KUWAITA CHADEMA NYUMBU SIO SIASASA ZA KISTARABU ASEMA POLEPOLE

Picha
Hamphrey Polepole akataa matumizi ya neno "NYUMBU" kwa wanaccm kumaanisha CHADEMA, na kusema CCM mpya ni pamoja na siasa za kistaarabu. Amesema hayo katika ukurasa wake wa twitter alipokuwa akitweet juu ya dhana ya Mabadiliko ndani ya ccm. Ndipo mmoja wa wanaccm alipochangia kwa kusema "Hakika nadhani wengi hawajalifahamu hili...endelea polepole kazi yako ni nzuri nyumbu watakoma" Nimekuwekea hapa chini tweet husika...

Waziri wa Fedha na Mipango azungumzia ukuaji wa uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai – Disemba, 2016

Picha
Nashukuru kupata fursa ya kuzungumza nanyi  leo kuhusu hali ya uchumi wa Taifa kwa kipindi cha Julai – Desemba, 2016 na matarajio hadi Juni 2017. Nitajitahidi kutumia lugha rahisi ili wananchi wa kawaida waweze kuelewa mambo ya msingi kuhusu mwenendo wa uchumi wa nchi yetu. Ustawi wa Uchumi Unapimwaje? Ustawi wa uchumi wa Taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mbalimbali. Kwa kifupi, ustawi wa uchumi unapimwa kwa kuangalia kama shughuli mbalimbali za kiuchumi zinaongezeka au zinapungua au kama zimedumaa.   Shughuli  muhimu zinazoangaliwa ni pamoja na uzalishaji wa chakula na mazao mbalimbali ya kilimo, mifugo na uvuvi; uzalishaji wa bidhaa za viwandani na migodini; ujenzi wa miundombinu; uwekezaji; mwenendo wa bei, biashara na masoko; utoaji wa huduma mbalimbali kwa jamii ikiwa ni pamoja na elimu, afya, maji, mawasiliano, usafiri na usafirishaji, utalii na huduma za kifedha; na kiwango cha utekelezaji wa bajeti ya Serikali.   Aidha, uchambuzi na tathmini...

RAPA NAY WA MITENGO AMSHUSHA PRESHA MPENZI WAKE

Picha
Msanii wa muziki wa hip hop Nay wa Mitego ameamua kuweka mambo sawa kwa mpenzi wake baada ya kuzagaa picha katika mitandao ya kijamii zinazomuonyesha rapper huyo kama amefunga ndoa. Rapper huyo amedai alikuwa hana maelewano na mpenzi wake kutokana na picha hizo. Kupitia Instagram, Nay wa Mitego ameandika: Na Shemeji yangu Mrs Allen Peter Kasiga. Yangu inakuja soon  hizi Picha zimefanya Mke wangu mtarajiwa Aone Kama nimeoa Mwanamke mwingine kimya kimya, maelewano hamna tenaaaa. Imenibidi tu ni Post kurudisha Amani ya Mahusiano yangu.! Wanao Post cjui nimeoa.. Tafadharini cjaoa bado Mtakuja kufanya watu wakafa bureee kwa Pressure…!! #sijiwezi LINK ON MY BIO Nay kwa sasa anafanya vizuri na wimbo ‘Sijiwez CHANZO:BONGO5

HARMONIZE ACHAGULIWA NA RAIS KIKWETE KWENDA KUWABURUDISHA NYUMBANI KWAO SIKU YA KUUAGA MWAKA

Picha
Hongera @harmonize_tz kwa kuchaguliwa kuburudisha katika hafla ya Kuukaribisha Mwaka Mpya Nyumbani kwa Mh Rais Mstaaf mh Jakaya Mrisho Kikwete, Msoga 31 dec 2016… Make us proud   @harmonize_tz

Tanzania yapaa kiuchumi kusini mwa Jangwa la Sahara

Picha
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema Tanzania imebaki kuwa miongoni mwa nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara Barani Afrika, ambazo uchumi wake unakua kwa kasi. Dk Mpango alisema hayo jijini Dar es Salaam jana, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uchumi wa taifa kwa kipindi cha Julai hadi Desemba, 2016 na matarajio hadi Juni, 2017. Alisema ukuaji wa uchumi ni mojawapo ya vitu vinavyotazamwa katika kutathmini afya ya uchumi wa taifa. Akifafanua, alitoa mfano kwa baadhi ya nchi hizo kuwa mwaka jana Tanzania uchumi wake ulikuwa kwa asilimia 7.0 na mwaka huu unakua asilimia 7.2, Kenya mwaka jana ulikua asilimia 5.6 na mwaka huu unakua asilimia 6.0, Uganda mwaka jana ulikuwa asilimia 4.8 na mwaka huu unakuwa asilimia 4.9. “Kwa mifano hiyo tunaona Tanzania imeendelea kufanya vizuri uchumi unakuwa kwa kasi kubwa katika Bara la Afrika,” alisema. Kwa upande mwingine, alisema kuwa ustawi wa uchumi wa taifa unapimwa kwa kuangalia viashiria mb...

Kamanda Sirro Katoa Tathmini ya Uhalifu Dar kwa Mwaka Mmzima wa 2016

Picha
KIKOSI cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, imekamata jumla ya watuhumiwa 13,626 na kuwafikishwa mahakamani kwa tuhuma mbalimbali, ikiwemo dawa za kulevya na ujambazi wa kutumia silaha kwa kipindi cha mwaka mmoja wa 2016. Aidha, hali ya uhalifu wa kutumia silaha katika jiji la Dar es Salaam umepungua, ukilinganisha na mwaka uliopita wa 2015 na matukio yanayoongezeka kwa wingi ni ya ubakaji na ulawiti. Akitoa tathmini ya mwaka mmoja, Kamishna wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro alisema jana kuwa matukio ya unyang’anyi wa kutumia silaha yamepungua kutoka 204 mwaka jana hadi 127 mwaka huu. Idadi hiyo ni pungufu ya matukio 77, sawa na asilimia 37.7 huku matukio ya kutumia nguvu yamepungua kutoka 1,181 mwaka jana hadi 874 sawa na asilimia 26. Kamishna Sirro alifafanua kuwa matukio ya mauaji, yamepungua kwa asilimia 11 ukilinganisha na mwaka jana, ambapo kulikuwa na jumla ya matukio 327 wakati kwa mwaka huu ni matukio 291 pungufu ya matukio 36. Alisema matuk...

MAN FONGO ASEMA BILA YEYE HAKUNA SINGELI

Picha
Msanii wa Singeli Man Fongo ambaye aliibuka mshindi katika tuzo za #EATVAwards kama msanii bora anayechipukia amefunguka na kusema kuwa hakuna muziki wa kisingeli bila yeye. Man Fongo alisema hayo kupitia kipindi cha eNEWZ na kusema kutokana na mapenzi aliyopata kutoka kwa mashabiki na kumuwezesha kupata tuzo ya #EATVAwards ameamua kuwashukuru mashabiki kwa kufanya show ya bure leo ambayo itafanyika kwa Ali Maua. "Mungu mkubwa nashukuru kupata hii tuzo kwani sikuwepo nilikuwa India lakini kwa kuwashukuru mashabiki wangu nimeamua leo tarehe 30 kufanya show ya bure ili nijichanganye na watu wangu wa uswahilini na kufurahia ushindi huu. Bila ya mimi hakuna kisingeli ila kwenye show yangu leo utaweza kuona wasanii wengine wengi wa Singeli ambao pia wanafanya vizuri hivyo watu waje kwa wingi washuhudie vipaji vingine". Alisema Man Fongo

ANGALIA PICHA ZA RAPA AKA ALIVYO MLETA MPENZI WAKE UKWENI

Picha

RIPOTI:GEORGE MICHAEL ALIKUWA ANA NDOTO ZA KUITWA BABA MWAKANI

Picha
Ripoti mpya imeibuka kuwa mwanamuziki wa Uingereza, George Michael aliyefariki ghafla siku ya Christmas alikuwa na mipango ya kuitwa baba kuanzia mwakani. Chanzo kimoja kimeiambia Daily Star kuwa muimbaji huyo aliyefariki akiwa hana mtoto hata mmoja alikuwa na ndoto za kuitwa baba kwa hiyo aliweka mipango ya kutafuta hata watoto wa kuwaasili kuanzia mwakani. “George’s dream was to be a father. He wanted to adopt or use a surrogate. It was his big aim, supported by Elton and David all the way. When Elton took the step, George knew he too had at last moved into that part of his life. To not have his own family, he felt incomplete,” kimesema chanzo hicho. “It was a missing link he craved. George always wanted to be a father, he wished his mother were alive to see the day. To start a family was on his to-do list for 2017,” kimeongeza. Staa huyo amefariki na kuacha utajiri wa paundi milioni 100 na watoto wa rafiki zake wa ubatizo, dada zake wakubwa na boyfr...

Habari Zilizopo Katika Magazeti ya Leo Jumamosi ya Disemba 31

Picha