Rais Dk. John Pombe Magufuli leo Desemba 29 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani humo na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.
Rais Magufuli pamoja na kuwapa pole wafiwa na wananchi wa Chato kwa kuondokewa na mpendwa wao pia ameitaka familia ya mzee Manyama kuendelea kuishi kwa kushikamana na kupendana kama ilivyokuwa enzi za uhai wa marehemu na kuwataka kuepukana na mifarakano.
Aidha Rais Magufuli amemuelezea Marehemu Mzee Manyama aliyefariki akiwa na umri wa miaka 80 kuwa alikuwa maarufu kijijini hapo na miongoni mwa mafundi hodari wa kushona nguo ambaye pia alimshonea sare zake za shule. Msemaji wa familia amemshukuru Rais Magufuli na ujumbe alioambatana nao kwa kuwafariji