SASA UNAWEZA DOWNLOAD T MEDIA NEWS APPS.

Alhamisi, 29 Desemba 2016

T media news

MKUU WA MKOA WA SIMIYU AMALIZIA MWAKA GAMBOSHI,NI KIONGOZI PEKEE WA SERIKALI ALIYEGUSA ENEO HILO MAARUFU IKULU YA WACHAWI

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka (Kulia) akiwa ameambatana na Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabato Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, wakati akiingia katika kijiji maarufu nchini Gamboshi 'Gambosi' kilichopo wilaya ya Bariadi Mkoani humo, ambapo Mtaka amekuwa Mkuu wa Mkoa wa Kwanza nchini kufika katika kijiji hicho tangu kianzishwe.

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Antony Mtaka akiongea na wananchi wa Kijiji maarufu nchini Gamboshi 'Gambosi' kilichopo wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, ambapo Mkuu huyo wa Mkoa amekuwa kiongozi wa kwanza mkuu ngazi ya Mkoa kufika katika kijiji hicho, ambapo alifika kwa ajili ya kuongoza harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2013.

Umati wa wananchi waliohudhuria mkutano huo wa harambee

Diwani kata ya Gambosi Bahame Kaliwa akizungumza

Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabato Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, ambaye ni mzaliwa katika kijiji hicho maarufu nchini Gambosi, akiongea na wananchi wa kijiji hicho wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi.

Wakazi wa Gambosi

Askofu Mkuu Kanisa la Waandventisti Wasabao Jimbo kuu la Kusini Mwa Tanzania Mark Malekana, ambaye ni mzaliwa katika kijiji hicho maarufu nchini Gambosi, akiongea na wananchi wa kijiji hicho wakati wa harambee ya kuchagisha ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi.

Kulia ni mzee maarufu katika kijiji cha Gambosi Shabani Masuka, (kushoto) ni Paroko wa parokia ya Ngulyati John Nkinga.


Wananchi wakiwa kwenye mkutano.

Magari yaliyowashangaza wananchi wa kijiji hicho, ambapo kila mmoja alibaki na mshangao kwa kile kilichoelezwa hakujawahi kufika msafara mkubwa wa magari kama hayo. 

********



"Gambosi" maarufu Gamboshi ni kijiji kinachopatikana katika wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kabla ya kuundwa kwa mkoa wa Simiyu, awali kilikuwa mkoa wa Shinyanga. 

Ni kilometa zaidi ya 30 kufika katika kijiji hicho kutokea mjini Bariadi.

Gambosi/Gamboshi ni kijiji kinachofahamika kwa historia kubwa hapa nchini, kinafahamika kama kijiji cha Wachawi, Ikulu ya wachawi nchini.

Tangu kuanzishwa kwa kijiji hicho hakuna kiongozi yeyote wa mkoa ambaye amefika kijijini hapo.

Kutokana na historia yao ilikuwa vigumu kwa wakuu wa mikoa kufika katika kijiji hicho, lakini juzi mwanga ulionekana kwao, baada ya mkuu wa mkoa wa Kwanza Antony Mtaka kufika kijijini hapo.

Ilikuwa siku njema na maalumu kwa wakazi wa kijiji hicho, ulikuwa ugeni mkubwa kwao, wa kushangaza machoni mwao, ilikuwa mwanga mkubwa kwao.

Mtaka alifika kijijini hapo kwa mara ya kwanza, na kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza kufika kijijini hapo, ambapo alifika kwa ajili ya kuongoza harambee ya ujenzi wa shule ya sekondari Gambosi ambayo ujenzi wake ulikwama tangu mwaka 2013.

Mtaka alikuwa ameambatana na Askofu Mkuu wa kanisa la Wasabato jimbo kuu la kusini mwa Tanzania ambaye ni mzaliwa wa kijijini hapo Mark Malekana, pamoja na wafanyabiashara wa mjini Bariadi.

“ Leo ni bahati kubwa sana kwa wananchi wa kijiji hiki, haijawahi kutokea kuingia msafara mkubwa wa magari kama haya, tena kiongozi ni mkuu wa mkoa kuja hapa Gambosi!! hii ni bahati kubwa sana kwetu, na ni kama maajabu kwetu, kutokana na historia mbaya iliyotuzunguka” ,walisikika wananchi hao wakiongea.

Katika harambee hiyo shilingi milioni 21.7 pamoja na vifaa mbalimbali vya ujenzi ikiwemo saruji mifuko 604, nondo pisi 100, madawati 80, vitabu 18 na mabati 20.

Mkuu wa mkoa wa Simiyu Anthony amefika katika kijiji cha Gambosi siku chache tu mwaka 2016 baada ya Askofu wa kanisa katoliki jimbo la Shinyanga mhashamu Liberatus Sangu kufika katika kijiji hicho na kuanzisha kanisa.